Blogger Widgets

Newdeal Africa

Tuesday, February 11, 2014

Wizara kutengeneza Database ya Diaspora kwa kushirikiana na IOM

Wizara kutengeneza Database ya Diaspora kwa kushirikiana na IOM

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo akizungumza wakati wa kikao kuhusu uundwaji wa Database na Tovuti kuhusu masuala ya Diaspora. Kikao hicho kiliwashirikisha Wajumbe kutoka Ofisi ya Rais Zanzibar, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uhamiaji na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji hapa nchini (IOM).
Wajumbe kutoka IOM, Ofisi ya Rais Zanzibar na Uhamiaji wakimsikiliza Bibi Jairo (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho
Mwakilishi kutoka IOM, Bi. Mia Immelback akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Bibi Jairo (wa pili kulia) akiwa na Wajumbe wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Mwakilishi wa IOM (hayupo pichani). Kutoka kushoto ni Bw. Mkumbwa Ally, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasialiano katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Kalumuna, Mkuu wa Kitengo cha ICT, Wizara ya Mambo ya Nje na Bi. Susan kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.
Bw. Kalumuna akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Picha na Reginald Kisaka.

Saturday, October 19, 2013

TZ DREAM TEAM

The New York Tanzanian Community Dream Team is getting stronger and stronger. Who can beat us? DMV, Texas, Boston get ready. We are here to beat you all! Every Sunday at 11:00 am the team trains in Brooklyn. You are welcome to join us.

UGANDA:MSIBA : MWANAFUNZI WA KITANZANIA AFARIKI DUNIA NCHINI UGANDA

Marehemu Samweli Kahewwnga
Marehemu Samweli Kahewwnga Aliyekuwa Mwanafunzi Katika Chuo Kimoja Huko Nchini Uganda Alifariki dunia wiki iliyopita.Samweli Kahewanga Aliyekuwa Mwenyeji wa Songea aliyewahi kuishi Mikoa ya Morogoro na Dodoma Alifariki akiwa Masomoni Nchini Uganda.
Marehemu alizikwa  Jana Mkoani Dodoma.

Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi Amen

WASHINGTON DC: TAARIFA YA KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA MAUWAJI OMAR SYKES WASHINGTON DC

Eneo la tukio Washington DC ambapo Omar Sykes (picha ya ndani) aliuawa.
Photo Credits: National Review Online 
Jumanne wiki hii, idara ya Polisi Washington DC (Metropolitan Police Department) ilitangaza kukamatwa kwa mtuhumiwa mmoja kati ya wawili waliokuwa wakitafutwa kwa mauaji ya mwanafunzi mTanzania aliyekuwa akisoma katika chuo kikuu cha Howard hapa jijini. 
Omar Sykes (22) aliuawa usiku wa Julai 4 mwaka huu nje kidogo ya maeneo ya chuo hicho alipokuwa pamoja na mwenzake.  
Wakiwa mtaa mmoja toka chuoni, wanafunzi hao walivamiwa na watu wenye silaha waliotaka kuwapora, na katika harakati hizo, Omar alipigwa risasi kifuani na kufariki.

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM). 

WAZIRI WA KILIMO, MHE. CHRISTOPHER CHIZA KUKUTANA NA WATANZANIA LONDON

Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Christopher Chiza 
Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania London unawakaribisha Watanzania wote watakaoweza kupata fursa kuja kuzungumza na Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Christopher Chiza na Wawakilishi kutoka SAGCOT hapo Ubalozini siku ya Jumatano (tarehe 23 Octoba 2013) kuanzia saa Kumi na Moja jioni (17:00).

Mheshimiwa Waziri anatarajiwa kuzungumzia masuala mbalimbali ya Kilimo, fursa zilizomo katika kilimo na ushirikishwaji wa Diaspora katika uwekezaji katika sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya nchi. Aidha Mhe. Christopher Chiza anatarajiwa kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wananchi watakaohudhuria mkutano huo.

IMETOLEWA NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA, LONDON

Monday, August 26, 2013

TUANZIE WAPI? TUANZIE WAPI?

Lengo kuu la maandishi yangu siyo kutaka kubadilisha mambo,bali napenda kusikiliza rai tofauti  na marekebisho toka kwa ndugu na marafiki wataosoma uchambuzi wangu ambao ulikuwa umenikaa kooni muda mrefu na nilikuwa natafuta nafasi ya kuumwaga hadharani kwa wenzangu wenye mtazamo mzuri zaidi waweze kunisahihisha ili nami nizinduke.
Baada ya kuangalia kwa utulivu jinsi maamuzi na mabadiliko yanavyofikiwa katika nchi zetu za kiafrika na sehemu nyingi duniani , nimefikia kukinaika ,kuna makundi matatu makuu yanayotuongoza au yanayotusukuma kufikia maamuzi fulani. Na kila kundi lina sifa na nguvu za kuathiri zinazotofautiana na kundi jingine. SIZUNGUMZII INDIVIDUALS WALIOMO NDANI YA MAKUNDI HAYO BALI NAZUNGUMZIA MAKUNDI AS MECHANISM.
Kundi la kwanza :WANASIASA
Kundi la pili:MATAJIRI WAKUBWA(Siyo wajasiriamali wala wanauchumi)
Kundi la tatu: VIONGOZI WA DINI. Siyo dini ni “VIONGOZI WA DINI” yoyote anayoiamini kila mmoja wetu.
Kila kundi lina sifa na mfumo tofauti na jingine . Kati ya kundi  la kwanza na la pili kuna kijikundi kina nguvu za ajabu, kikundi hiki ni cha “USALAMA NA UPELELEZI”. Aidha kuna kijikundi kingine cha WACHUNGA MASLAHI”. Wahusika wa kikundi hiki hujihusisha na kujiingiza katika makundi yote matatu kulingana na hali ya maslahi itavyowavuta. Kijikundi hiki ni hatari mno, hakina simile katika kuhakikisha wanafanikisha kile wakitakacho au kile walichotakiwa wakifanye ili mradi lengo likamilike.Tofauti muhimu iliyopo kati ya kijikundi hiki na wale MATAJIRI WAKUBWA ni kuwa wahusika wa kijikundi hiki HUJIFICHA  na huonekana tu matunda ya vitendo vyao.Wachache hujulikana baada ya mibiginyo inayofanywa ili pia kulinda maslahi makuu.
NB. Sikutaja kundi la WANAJESHI ambao kila demokrasia inavyozidi kukua Afrika wanajikuta ni kundi la kutekeleza maamuzi ya wanasiasa - hata kama hawakubaliani nayo-(WITH EXCEPTION OF EGYPT RECENTLY) tofauti na miaka ya nyuma  walipokuwa wakifanya mapinduzi ya mara kwa mara. Aidha sikutaja vyombo vya habari ambavyo vyote vipo chini ya MATAJIRI WAKUBWA au WANASIASA . Ama wale wanaojiita wanablogs wao nawaweka katika kundi la “WACHUNGA MASLAHI” kwani ni wachache mno kati yao wanaoelezea fikra zao huru.
Kundi la kwanza : WANASIASA.
Sifa kuu za kundi hili ni: UONGO NA KUBADILISHA MISIMAMO
Hakuna kiongozi yeyote duniani aliyetekeleza kikamilifu yale yote aliyoyaahidi kabla ya kuchaguliwa kuwa kiongozi.Ajabu ya mambo sisi waongozwa kila siku tunawataka wawe wakweli na wasibadili misimamo!!!Nadhani kuna sababu ya wazi inayowalazimu wajivishe sifa hii, sababu ambayo sisi waongozwa daima haitugusi katika maisha yetu ya kila siku,Sababu hiyo ni kuwa wanapoingia madarakani hukumbana na mibiginyo na facts tofauti zinazowalazimu wabadilishe misimamo yao ili waweze kuendeleza kuwa Viongozi. Mibiginyo hii inamkumba kila kiongozi bila kujali ukubwa na nguvu ya nchi anayoiongoza!!
Kila mmoja anaweza kuihisi hali hii katika nafasi yoyote ya uongozi wa kijamii aliyowahi kuisimamia.


Kundi la pili : MATAJIRI WAKUBWA.
Sifa kuu za kundi hili ni : KUPATA WAKITAKACHO BILA KUJALI NJIA ILIYOTUMIKA
Hawa ni watekelezaji wakuu wa Machiavellism “End justifies the means” . Ukiangalia kwa makini vita na maafa mengi duniani yamechochewa na kundi hili ambalo lina nguvu kubwa  ya kichinichini katika kulilazimisha kundi la kwanza (wanasiasa )ili lichukue maamuzi yatayolingana na matakwa na maslahi yao.
Hili ni kundi pekee ambalo wahusika wake HAWAJIFICHI  katika kuhakikisha wanapata wakitakacho.Misimamo yao ipo wazi mno na wala haina mizunguko.Hawatumii unafiki wa maadili  kama wanavyofanya wahusika wa kundi la kwanza (wanasiasa)na wa kundi la tatu “A” kama tutavyoona hapo mbele.
Kundi la tatu :VIONGOZI WA DINI.
Kundi hili linagawanyika katika sehemu mbili kuu.”A” na “B”.Kundi la .”A”ni lile la wale wanaotumiwa kwa maslahi ya WANASIASA NA MATAJIRI WAKUBWA.Ama kundi la “B”.ni lile la wale wachache wanaojaribu kufuata dini bila kujali maslahi ya kundi la kwanza wala la pili.Mara zote kila mmoja hudai kuwa yumo katika kundi la “B”.Ila huwa si tabu kuwagundua wapi walipo na hasa kama watatakiwa watoe maamuzi yatayopingana na maslahi ya WANASIASA au MATAJIRI WAKUBWA.
Sifa kuu za kundi la tatu “A” ni :KUWALAGHAI WAUMINI.
Wahusika wa kundi hili, ndani ya nyoyo  zao wana misimamo ya kundi la  kwanza na la pili ila wanapokutana na waumini wao hujilazimisha waonekane kama wapo pamoja nao kumbe sivyo!!!
Sifa kuu za kundi la tatu “B” ni: KUJITENGA AU KUTENGWA.
Wahusika wa kundi hili wamejigawa katika sehemu mbili.Ya kwanza ni wale waliokwisha gundua kuwa hawawezi kufikisha mafunzo halisi ya dini zao bila kuingiliwa na makundi makuu niliyokwisha  taja hapo nyuma na matokeo yake huamua KUJITENGA na kutekeleza dini zao bila marumbano.Ama sehemu ya pili ni ile ya wale wanaoendelea kuamini kuwa wana nafasi ya kuweza kufikisha mafunzo halisi kwa waumini wao na huendelea kupambana na makundi makuuu na mara nyingi hufikia KUTENGWA ili wasiharibu maslahi ya wengine!!!

MWISHO nafungia kwa imani ninayoiamini kwa dhati kuwa tumekuja duniani miaka kadhaa iliyopita na kila mmoja ataondoka baada ya miaka kadhaa na kuiwacha dunia ikiendelea kama ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita. Katika kipindi hiki cha miaka kadhaa tunayoishi HATUNA UWEZO WA KUBADILISHA DUNIA BALI tuna uwezo wa kujaribu KUREKEBISHA BAADHI YA MACHACHE YANAYOTUZUNGUKA KATIKA JAMII ZETU.

JE TUANZIE WAPI?

TUANZIE HAPA  (…………..KUANZA KUJITAMBUA NA KUONDOKANA NA FIKRA HASI ZILIZOPANDIKIZWA KATIKA VICHWA VYETU(kwa maslahi ya wachache) KWAMBA SISI WAAFRIKA MUNGU KATUUMBA TUBAKI KATIKA UNYONGE NA UDHALILI  HADI SIKU YA KIYAMA.)TUSITAKE MABADILIKO YA GHAFLA(ambayo hutukatiksha tamaa tunaposhindwa kuyafikia) TUANZE KWA KUREKEBISHA MACHACHE NA KUSIFU KILA JEMA LINALOFANYIKA KATIKA JAMII ZETU.HATA KAMA LITAFANYWA NA TUSIYEMPENDA.

KAYU LIGOPORA
ATHENS – GREECE
27 AUGUST 2013

Wednesday, July 3, 2013

Mtanzania ajinyonga nchini Urusi!


20130702-130838.jpg

Habari ambazo  zlizopatikana  kutoka kwa baadhi ya Watanzania waishio Saint Petersburg, Urusi, ni kwamba Mtanzania aliyeweka makazi yake mjini hapo kwa muda mrefu Ndg. Shabani Japhari ameaga dunia kwa kujinyonga.
Akituma ujumbe huo kupitia mtandao wake wa Facebook, Ndg. Moses Mango, ambaye pia ni mkazi wa muda mrefu wa Mji huo, alisema ” I hate bringing bad news. Kama wengi mlivyosikia, ndugu yetu Shabani ametutoka leo asubuhi kwa kujinyonga. Kwa sie wote hapa, huu ni mzigo mzito sana aliotuachia. Ningeomba wote tuwe pamoja katika kukamilisha shughuli zote zinazotokana na msiba huu. RIP mrefu“, alimalizia kusema Ndg. Mango.
Shabani alifika Urusi miaka ya 80 kama mwanafunzi, na baada ya kuhitimu masomo yake, alibaki mjini Saint Petersburg na kuendelea kujihusisha na masuala mbalimbali ya biashara. Vijana wengi waliokuwa wakifika Urusi ki masomo walimuheshimu na kumchukulia kama kaka, na wengine kumtaka ushauri katika masuala mbalimbali kutokana na uzoefu wake wa Mji.
Marehemu Shabani, ameacha mke na watoto Kandhaa, na dua zetu tunazielekeza kwa familia hiyo, na familia yake nyingine kubwa, iliyopo Tanzania. Kwa hakika wote tumeshtushwa na msiba huu, ambao bado umetuacha na maswali mengi, bila majibu.

Wednesday, May 1, 2013

GERMANY: Sherehe za miaka 49 ya muungano wa Tanzania!

Siku ya Jumamosi tarehe 27.04.2013 Watanzania wanaoishi Ujerumani, chini ya mwamvuli wa umoja wao (UTU) waliuhakikishia ulimwengu kuwa neno "MUUNGANO" lina maana kamili kwa maisha ya  Mtanzania na binadamu wengine.
Sherehe hizo zilizowakusanya Watanzania na marafiki wa Tazania kutoka kila kona  ya Ujerumani, ziliutingisha mji wa Cologne katika usiku usiokwisha wa kusherehekea miaka 49 ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Ali Siwa Naibu balozi wa Tanzania nchini Ujerumani alikuwa mstari wa mbele akiwaongoza Watanzania katika Muungano Day.
Wasanii mbalimbali walitumbuiza jukwaani na kuipeperusha vilivyo bendera ya Tazania.
Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania ujerumani Mh.Mfundo na kamati yake wameahidi kufanya mambo makubwa na kuitangaza  Tanzania kwa hali na mali chini  ya  Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU)
kwa pich zaidi   gonga Hapa

Friday, April 26, 2013

TANGAZO LA MSIBA NEW JERSEY-USA

TAFADHALI SAIDIA  KUTO ATAAEIFA KAMA UNAWAJUA NDUGU WA MAREHEMU


Tunaomba mtupostie tangazo hili katika blog zenu kama blog yako ni ya habari mbalimbali. Kuna kijana amefariki New Jersey, USA. Kijana aliyefariki alinajulikana kwa jina la Adolf, Brian au Tadeous Rwekagende. Alikua anasema alisoma Tambaza na alikua na mdogo wake anaitwa Rodrick Rwekagende ambaye naye alikua anaishi Texas. Ila cha kusikitisha ni kuwa huyo mdogo wake alisema alifariki mwaka jana mwezi wa nne (Tanzania).

Adolf alikua anasema baba yake na mama yake walifariki yeye na mdogo wake huyo wakiwa wadogo. Sasa yeye alikulia kwa mjomba wake. Juzi Adolf alipata massive stroke na kulazwa st Barnabas hospital, Livingston, NJ na kufariki. Mpaka sasa hivi kuna watu wametafuta ndugu zake na kumpata mjomba wake mmoja huko Bukoba vijijini. Hatukuweza kupata ndugu wa karibu hapa marekani na mpaka sasa hivi maiti yake ipo hospital haijawa claimed. Hivyo kama binadamu tumeamua kujichangisha ili tuweze kupeleka mwili wa mwezetu Tanzania kwa mazishi. Gharama za kuzika huku na kusafirisha kupeleka Tanzania ni karibu sawasawa tu hivyo tunaona ni bora akapumzike na ndugu zake Tanzania.

Hivyo tunaomba mtupostie kwenye blog zenu hili tangazo liwafikie watanzania watakaopenda kumsaidia ili apelekwe Tanzania tutashukuru sana. Tumefungua mahali pa kuchangisha helahttp://www.donationto.com/adolfsendhomecost au kama mtu anatumia paypal account ni adolffuneralcost@gmail.com. Tutawapa majina ya watu watakaokua kwenye kamati ya kukusanya hela mara tutakapomaliza kikao tunachotegemea kufanyika Jumamosi. na hela zote zitaonyeshwa zilivyotumika kama zipo extra zitapelekwa huko kwa wajomba zake Bukoba.

Na kama kuna mtu ana picha yake basi mtutumie kwa sababu hakuna mtu aliye na picha yake. ID yake ipo hospital hawawezi kumpa mtu mpaka wakishajua nani anachukua mwili na mahali alipokua anaishi hawaruhusu mtu kuingia kwa sasa mpaka wakishajua mazishi ni wapi au ndugu wa karibu ni wapi. Hivyo hamna mtu ana picha yake..

Please sisi hapa tunajitahidi ili azikwe kama ubinadamu hivyo huu sio muda wa kuanza kuuliza maswali kwa nini hiki wala kile...Kwa vile hata sisi tuna maswali mengi na hakuna mtu mweye jibu....Tunachojua ni kuwa alipata massive stroke na amefariki na hakuna ndugu yake wa karibu huku marekani.

Tunatanguliza shukurani na pia kama blog yako hupost mambo ya habari tunaomba utusaidie kuforward hii email kwa watu wengine...Kuna wazee wako NY kama wakikukubali kushughulikia huu msiba tutawatangazia na kuwapa information mpya. Na hela zitakazopatikana zitahamishiwa kwenye fund yeyote watakayofungua kama wataamua kufungua mpya au wataamua kuendelea na hi hii. Tunachotaka ni kusafirisha kijana wa watu Tanzania kwa sababu sasa hivi hilo ndio lengo letu....na hakuna mtu yeyote aliyesema kitu chochote hivyo kama kikao kikifanyika basi tutawaeleza linaloendelea.

Nitajitahidi kuupdate kinachoendelea katika twitter handle yangu @swahilimom
Regards,
Pauline

Thursday, April 4, 2013

UCHAGUZI JUMUIYA YA WATANZANIA GREECE

JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI ILIFANYA UCHAGUZI WAKE MKUU WA KUCHAGUA VIONGOZI NA WAJUMBE WA JUMUIYA HIYO SIKU YA JUMAMOSI TAREHE.23/04/2013, UCHAGUZI HUO ULISIMAMIWA VIZURI NA TUME MAALUM ILIYOCHAGULIWA CHINI YA MWENYEKITI WAKE OMAR HUSSEIN MILALA NA WAJUMBE WAKE WA 4.WATANZANIA WENGI WALIJITOKEZA KATIKA KUTUMIA HAKI YAO HIYO YA KUCHAGUA VIONGOZI AMBAO KWA RIDHAA ZAO WALIAMUA KUWACHAGUA.

M/KITI: HASSAN OMAR CHUNDA
MSAIDIZI M/KITI: SALUM MSELLEM SURURU
KATIBU: SAID MADUBEI
MSAIDI KATIBU: FRANCIES WILLIAM
MSHIKA FEDHA:SAID MOH'D SAID ( NURAMO)
MSAIDIZI:OMAR KITWANA KOPA

WAJUMBE
1: WILLIAM MUKONY
2:SULEIMAN KHAMIS MASOUD
3:AHMEID MSELLEM SURURU
4:SAID VURU.

JUMUIYA INATOA SHUKRANI ZA THATI KWA WALE WOTE WALIOJITOKEZA KATIKA UCHAGUZI HUO AMBAO ULIMALIZA KWA SALAMA, PIA INAWAOMBEA KILA LA KHERI NA AFYA NJEMA VIONGOZI WOTE WALICHAGULIWA NA UTEKELEZAJI MZURI WA MAJUKUM YAO,PIA SHUKRANI ZAID KWA TUME YOTE ILIYOSIMAMIA UCHAGUZI MZIMA.

Wednesday, April 3, 2013

Watanzania Ujerumani Kusherekea Miaka 49 ya MuunganoWatanzania Ujerumani kusherekea miaka 49 ya Muungano
UMOJA wa Watanzania Ujerumani (UTU) unatarajia kufanya sherehe za miaka 49 ya Muungano
wa Bara na Visiwani, kama linavyoonekana tangazo unatarajia kufanya sherehe hizo Mjini Kolon,
Siku ya Jumamosi 27.04.2013. Watanzania wote na marafiki wa Tanzania mnaoishi ndani na nje Ujerumani mnakaribishwa.
“Umoja ni Nguvu! Utengano Ni Udhaifu” Chereko Chereko na mwenye mwana Watanzania jitokezeni kwa wingi. Kwa mawasiliano zaidi at kamati.utu@googlemail.com
simu +49(0)1737363422

Saturday, March 30, 2013

Mtanzania afia Uwanja wa Ndege nchini China

KIFO CHA KITATANISHI CHA MBONGO CHINA!! NI KIZAAA ZAAAAA!!“Tangu alipofariki madaktari walisema ripoti ingetolewa baada ya siku saba ambazo ziliisha Jumatatu, mpaka sasa hiyo ripoti hatujaipata lakini Mwambata wa Elimu katika Ubalozi wa Tanzania
nadhani atakuwa ameipata kwa sababu ndiye alikuwa akiiwakilisha Tanzania
katika uchunguzi huo,”

 Mwanafunzi wa Kitanzania aliyekuwa akisoma katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Huazhong nchini China, Leonard Peter Tambalu amefariki dunia ghafla katika
mazingira ya kutatanisha wakati akiwa anajiandaa kurejea nchini.

Tambalu aliyekuwa mwaka wa pili katika chuo hicho kilichopo kwenye mji wa
Wuhan, alifikwa na mauti hayo Machi 17 mwaka huu wakati akiwa katika
Uwanja wa Ndege mjini Beijing. Marehemu alikuwa Ofisa Kilimo Mwandamizi
kutoka wilayani Iramba mkoani Singida.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Christina Midelo hakukubali wala kukanusha kuwapo kwa tukio hilo. “Sina taarifa za kifo cha kijana huyo, wanaoweza kuzungumza ni Ubalozi
wa China kwa kuwa ndio waliokuwa wakimsomesha.”
Balozi wa Tanzania nchini China, Philip Marmo, ambaye yupo nchini kutokana na ushiriki
wake katika mapokezi ya Rais wa China, Xi Jinping, alikiri kufahamu
suala hilo. Katibu wa Umoja wa Wanafunzi wanaosoma vyuo mbalimbali
katika mji wa Wuhan (Wtasa), Humphrey Sikauki, alithibitisha kifo cha Tambalu na kwamba mwili wake ulikuwa unafanyiwa uchunguzi na maofisa wa serikali ya China wakishirikiana na wale wa Tanzania.
Tangu alipofariki madaktari walisema ripoti ingetolewa baada ya siku saba
ambazo ziliisha Jumatatu, mpaka sasa hiyo ripoti hatujaipata lakini
Mwambata wa Elimu katika Ubalozi wa Tanzania nadhani atakuwa ameipata
kwa sababu ndiye alikuwa akiiwakilisha Tanzania katika uchunguzi huo,”
alisema Sikauki.
Gazeti hili lilijaribu mara kadhaa kuwasiliana na
Mwambata wa Elimu katika Ubalozi wa Tanzania nchini China, George
Manongi lakini mawasiliano yalikuwa magumu, kutokana kushindwa
kusikilizana.

Tuesday, March 19, 2013

BENDERA TA TANZANIA YAPEPEA VATICAN

Wadau wakipeperusha bendera ya Tanzania Vatican, ni baadhi ya Watanzania waliohudhuria  na kutuwakilisha  katika sherehe za  kupatikana Papa mpya.

SERIKALI YASHAURIWA KUTOA KIPAUMBELE KWA WATANZANIA WAISHIO NJE YA TANZANIA KATIKA UWEKEZAJI

 
Na Waandishi wetu-MAELEZO_Dar es Salaam.
Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano kimataifa imeshauri Serikali kutoa fursa kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi kuja kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali ili kukuza uchumi wetu.

Kauli hiyo imetolewa leo na wajumbe wa Kamati hiyo ilipokutana na
viongozi waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Kimataifa
ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya bajeti ya mwaka 2013/2014

Walisema wakati umefikwa kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi kutowekewa vikwazo katika kupata taarifa muhimu zinazohusu sekta mbalimbali za uchumi ili waweze kuja kuwekeza badala ya fedha zao kukaa nazo nje ya Tanzania.

Waliongeza kuwa ni vema Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ikaunda
Kitengo maalum cha diplomasia ya uchumi kitakachoshirikisha wataalamu
wa sekta mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika utangazaji wa fursa za
uwekezaji nchini kwa ili kuboresha nyanja za uchumi kupitia Watanzania
waishio nje.

Akijibu baadhi ya hoja za wajumbe wa Kamati hiyo Naibu Waziri wa Wizara wa
Mambo ya Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Maalim alisema kuwa
Serikali hivi sasa inaendelea kutangaza fursa mbalimbali ambazo zipo
Tanzania ambapo tayari wawekezaji kutoka Oman wameshaonyesha nia ya
kuwekeza nchini.

Alisemakuwa wawekezaji hao wanakusudia kununua nyama ambapo pia watajenga
machinjio ya kisasa ambayo yatatumika kuchinjia mifugo kabla ya nyama
haijasafirishwa kwenda nje ya Tanzania.

KUTANA NA DRIZZLE DETECTIVE AGENCY

CONTACT Our main areas of work are: General investigation, Fraud Investigation, Personal Bodyguards Security services Management Consultancy, Technical Security Consultancy, Professionals Staff Vetting, and Risk Management. Contacts Old posts Office, Mkwepu Street Tel 0767999356, 0767999336, 0774444497 Email: info@drizzledetectiveagency.com

TEXAS-SEMINA YA WALIMU WA KARATE

Sensei Rumadha Fundi (Romi)( ( 3rd Dan black belt)
Sensei Rumadha Fundi (Romi)( 3rd Dan black belt),  akiwajibika katika semina ya karate Dojo ya Sugarland, Texas USA katika seminar ya walimu wa karate (ma-sensei) wiki iliyopita chini ya uongozi wake Sensei Ramon Veras (7th Dan), wa Traditional Okinawan Goju Ryu Karate-Do.
Sensei Rumadha ni  mmoja wa walimu wa Kitanzania wa karate ambao wanafanya vizuri katika fani hii  ughaibuni, ni matumaini yetu wahusika katika sekta ya michezo hasa upande wa mapambano kama ngumi, kick boxing, judo nk wataangalia uwezekano wa kupata mchango wao ambao unaweza kusaidia katika kuboresha wanamichezo wetu kufikia kiwango cha kimataifa na kuliletea sifa taifa letu.


GFAMILY
  Blogger.


Saturday, March 16, 2013

KIOTA KIPYA CHA MAPUMZIKO
TAI TANDIKA ANAWAKARIBISHA WATANZANIA WOTE NAPOLI BAADA YTA KAZI NA SIKU ZA WEEKEND KATIKA CLUB YAKE ILIYOPO PINETAMARE  VILLAGIO COPOLA KWA KILA IJUMAA KUANZIA SAA TATU USIKU KIINGILIO FREE!!!!!  WOTE MNAKARIBISHWA!!

Saturday, March 9, 2013

NEW PRIVATE INVESTIGATION FIRM IN TANZANIA

CONTACT ITS NEW IN TANZANIA! ITS DRIZZLE DETECTIVE AGENCY! A PRIVATE INVESTIGATION FIRM IN TANZANIA. Drizzle Detective Agency (DDA) is a Private Company established in 2010. Professions with a wide Experience in many fields namely Security Services, General Investigations and Fraud Investigation. Our firm has been fully Registered and Authorized with Ministry of Home affairs and conducting its Activities Accordance with all Applicable laws. Our main areas of work are: General investigation, Fraud Investigation, Personal Bodyguards Security services Management Consultancy, Technical Security Consultancy, Professionals Staff Vetting, and Risk Management. Contacts Old posts Office, Mkwepu Street Tel 0767999356, 0767999336, 0774444497 Email: info@drizzledetectiveagency.com

Friday, February 22, 2013MAONI YANGU KUHUSU MABADILIKO YA KATIBA

 Nadhani ingependeza kama nasi huku ughaibuni tungekuwa tunabadilishana mawazo kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya katiba(INGAWA KUNA WALE WANAOAMINI KUWA HATUNA TUNACHOWEZA KUBADILISHA.KILA KITU KIMESHAAMULIWA NA WAKUU WENYE SAUTI TANZANIA).
Mimi nilishayapeleka yangu www.katiba.go.tz.Na kama wengi wetu hawana wakati wa kueleza mengi , ni bora tujaze hili suala la URAIA PACHA Bila ya sisi huku ughaibuni kulipigia debe, huenda na wale wa nyumbani hata wasilikumbuke.
Maoni yangu yana sehemu nne kuu zifuatazo:

1. KINGA YA RAISI .


Anapokuwa madarakani asishtakiwe ila mara tu muhula wake wa kuongoza unapokwisha na siku anapoapishwa Raisi mpya,KINGA ya Raisi mstaafu ifutike automatically ili aweze kushtakiwa kwa makosa aliyoyafanya katika kipindi cha uongozi wake.Na ikipita miaka mitano tangu kumaliza uongozi na akawa hakushtakiwa kwa kosa lolote ,Kinga yake arudishiwe na kuanzia hapo hatoweza tena kushtakiwa.
(UCHAMBUZI )Viongozi wengi wa Afrika wanatumia vibaya mno madaraka yao wakijijua kuwa hawatoshtakiwa wanapotoka madarakani.Kuwepo kipengee hiki kutasaidia wapunguze ubadhirifu wanapokuwa madarakani.

2. WAFUNGWA:


a) HUKUMU YA KIFO ISIWEPO. Kwa kosa lolote HATA LA KUUA AU LA UHAINI.Hukumu ya juu iwe ni kifungo cha maisha.
(UCHAMBUZI )Tunapomuua tunakuwa tumempumzisha na wala hatohisi uchungu wa adhabu kwa lile kosa alilofanya.Mimi hapa wala silalii katika ile hoja ya HAKI YA MWANADAMU KUISHI wanayoitumia baadhi ya wale wanaopinga hukumu ya kifo duniani.
b)KITUMIKE KIFUNGO CHA NJE NA KAZI ZA KUNUFAISHA JAMII kwa makosa yasiyokuwa ya jinai,
(UCHAMBUZI ) Ndugu zetu wengi hupelekwa rumande kwa kuiba kuku na wanapotakiwa watoe dhamana wanashindwa na hurundikwa rumande na nchi hulazimika kuwahudumia bila faida yoyote.Kinachosikitisha wengi wanaokwenda rumande ni hawa ndugu zetu masikini wakati wale wenye uwezo wa kiuchumi (na hasa wageni)hulipa kiwango chochote wanachotakiwa na wanakuwa na uhakika wa kutokwenda jela.!!
c)IFUTWE CRIMINAL RECORD baada ya kupita miaka kumi tangu mfungwa kumaliza kifungo chake bila kufanya kosa jingine la jinai.
(UCHAMBUZI) Wafungwa wanapomaliza kifungo huwa wanabaki maisha yao yote katika records za INTERPOL kuwa ni criminals, na hii inawakosesha haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi katika jamii yao au hata kupata kazi kwa kuwa huonekana ni criminals.Hali hii inawafanya wengi warudie tena katika uharamia kwa sababu wanajihisi kuwa jamii haiwapi nafasi ya kubadilisha au kuifuta sifa mbaya ya u -crimial inayowaandama maisha yao yote kutokana na justice system ilivyo ya kidhuluma na uonevu duniani.3. MUUNGANO:

Kuwe na nchi inayoitwa ZANZIBAR ,
Kuwe na nchi inayoitwa TANGANYIKA (au jina lolote litalochaguliwa)
Kuwe na mfumo wa Muungano utaokubalika na pande zote mbili( Kazi hii tuwachie wataalamu siyo kila mtu anaiweza).

4. URAIA PACHA(DUAL CITIZENSHIP)

Raia waruhusiwe kuwa na uraia pacha
(UCHAMBUZI) Hapa sina haja ya kuchambua kwa sababu zinaeleweka wazi faida za uraia pacha na mifano ipo wazi kwa zile nchi zenye mfumo huu jinsi zinavyofaidika katika kila nyanja.HAKUNA hasara wala madhara ya kuwa na uraia pacha zaidi ya faida tu.

KAYU LIGOPORA
ATHENS

Tuesday, February 5, 2013

JE HATI YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR IPO?JE HATI YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR IPO AU HAIPO?

Katika elimu ya Mantiki kuna kanuni nyepesi za kuufikia ukweli,kuna kanuni nyepesi zinazoweza kumuongoza mtu kuelewa kirahisi ukweli ulipo na hasa kama kuna maelezo ya pande mbili zinazogongana. Lakini katika siasa HAKUNA KABISA KANUNI ZA KUUJUA UKWELI. Kwenye siasa maslahi na MACHIAVELLISM(End justifies the means) hutumika sana bila hata kumwogopa Mungu!!!!!Wakati mwingine viongozi wa siasa -ambao hujisahau na kujiona wana akili nyingi na busara kuliko wale wanaowaongoza- hufanya mambo ambayo hata mtoto wa miaka miwili hugundua wazi kuwa KUNA KASORO KATIKA MAELEZO WANAYOYATOA!!!
Utangulizi wa hapo juu unanifikisha moja kwa moja katika kulichambua jibu la swali tunalojiuliza wengi JE HATI YA MUUNGANO IPO?
RAIS SHEIN” anasema IPO(anaetaka anaweza kuiona UN.)
RAIS MSTAAFU KARUME” anasema HAJAWAHI KUIONA(Hakuwahi kuiona katika kipindi chote alipokuwa Rais)
Kwa wale waliozowea kuchezea maneno watahoji kuwa “KUTOIONA”does not necessarily mean kwamba “HAIPO”- Lakini inajionesha wazi kuwa anamaanisha “HAIPO”.
Kwa hiyo tuna viongozi wakuu wawili wenye maelezo yanayogongana:
A” anasema HATI YA MUUNGANO IPO.
B”anasema HATI YA MUUNGANO HAIPO
Je ukweli upo wapi kati ya maelezo ya “A” na ya “B?
Cha kusikitisha ni kuwa katika hatua za kuutafuta utatuzi, siyo tu kuhusiana na Hati ya Muungano bali hata katika kujadili suala la mfumo gani wa Muungano uwepo kati ya Wazanzibari na Watanzania bara) mara nyingi watu tumekuwa tukitumia sana emotion,michemko,hasira,to the extent watu kujihisi kama sisi ni pande mbili za maadui!!!!WAKATI KIUKWELI SISI NI PANDE MBILI ZA WANANDUGU.(Ukisoma rai zinazotolewa mitandaoni toka kwa wale wenye misimamo mikali wa pande zote mbili za Bara na Visiwani hutochelewa kuona wazi maelezo yanayovuka mipaka)


Kabla sijakamilisha maelezo yangu nina furaha kubwa kuyanukuu maelezo mazuri na ya busara yaliyoandikwa na Ashakh Kiongozi (Mzalendo.net)02/02/2013 11:07 alipokuwa akitoa ushauri wa jinsi gani ya kulipata jibu la Hati ya Muungano.Na hapa namnukuu :
Tukumbuke hata mahkama chini ya mwanasheria mkuu wa Zanzibar wakati huo Bw Iddi Pandu Hassan alithibitisha kwamba hajawahi kuuona na Serikali ya Zanzibar haina mkataba huo.
Naamini Dr Shein kasema kwa maana yake kuwa mkataba wanao. Sasa ni jukumu letu la kumwambia atuonyeshe na sie hapahapa Zanzibar bila ya kwenda NewYork.
Tutumie Njia za busara za kumwambia atuonyeshe, kama hivi:
1) Maalim Seif – yeye ni makamo athibitishe ukweli huu hasa kwa vile anakwenda na kuingia Ikulu.
2) Mh Aboubakar – Waziri wa Sheria athibitishe kwa mujibu wa sheria mkataba huu ulipo.
3) Othman Masoud – Mwanasheria yeye ndie nundu wa hili
4) Jaji OMar Makungu – Jaji Mkuu wa Zanzibar kisheria tayari wameshatoa maamuzi yao
5) Makachero – ni ukifika wakati ni lazima makachero wafanye kazi yao ili kutupa japo copy yake

Hii ni mbiu ya mgambo kutoka kwa Dr Shein, huu ndio mwanya mzuri wa kuuona mkataba wetu ikiwa tunao na upo.” Mwisho wa kumnukuu
Namalizia kwa kusema:
Mimi niandikaye maelezo haya natoka TANZANIA BARA . nimejitahidi na naendelea kujitahidi kutotumia michemko wala hasira katika kuielezea hali ya MUSTAKBAL WA MUUNGANO WETU ambao kwa kiasi kikubwa naamini vyovyote utakavyokuwa uamuzi wa maoni ya katiba mpya,(uwe wa mkataba uwe wa serikali 3 au 1) uamuzi huo HAUTOUFUTA UDUGU ULIOPO KATI YETU. Na hata kama kutakuwepo na wenye misimamo mikali toka pande zote mbili, watu hao hawatofanikiwa kupandikiza chuki katika nyoyo za wengi wanaopenda kusiwe na chuki kati yetu.
Nafunga maelezo yangu kwa kuwaomba wote tunaoishi ughaibuni TUSIATHIRIKE na michemko ya nyumbani tukawa tunaihamishia huku bila kuzingatia mazingira halisi ya mfumo wa maisha yetu ya huku.Mazingira ya huku yanahitaji zaidi mshikamano ,busara utulivu na kuvumiliana bila kujali wapi anatoka kila mmoja wetu.TUSICHANGANYE MAMBO TUTAKUJA VURUGA.
Namuomba Mola atulinde na atuzidishie hekima (Amin.)
                                                                                                   KAYU LIGOPORA
ATHENS GREECE.
kaygreko@yahoo.com  

Wednesday, January 30, 2013

UTUMWA WA KILEO


KAMA HAYA NI YA KWELI (Na sioni kwa nini watuongopee) BASI TUJUE TUMERUDI NYUMA SAAANA KUPITA HATA KILE KIPINDI CHA UTUMWA!!!!Je nini tufanye?( KAYU LIGOPORA)


Biashara ya binadamu imeibuka kwa kasi nchini na kutishia usalama wa nchi kutokana na watoto wenye umri kati ya miaka 8-15 baadhi yao wakiwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kusafirishwa...

Saturday, January 5, 2013

SERIKALI KUWATUMIA WATAALAMU WA KITANZANIA WALIOKO UGHAIBUNI (DIASPORA) NA NDANI YA NCHI KUJENGA UWEZO NA UFANISI WA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI MUHIMU ZA SERIKALI


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakusudia kuwatumia wataalamu wa Kitanzania walioko ndani ya nchi na wale walioko ughaibuni (Diaspora) katika kutekeleza mipango yake kadhaa yenye umuhimu kwa Taifa.

Hapo awali, Serikali iliwatumia zaidi wataalamu kutoka nchi nyingine, ambapo kwa sasa lengo ni kuona kwamba wataalamu wa nchi nyingine wanatumika pale tu ambapo wataalamu wa Kitanzania walio ndani na nje ya nchi hawajapatikana kufanya kazi husika.

Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali itapenda kupata wataalamu wa Kitanzania kwenye maeneo yafuatayo:-

                     (i) Mfumo mzima wa utafutaji, uchimbaji, uongezaji thamani na usambazaji wa gesi    asilia na mafuta.

                    (ii) Kuimarisha matumizi salama ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katikakuboresha utendaji wa Serikali na utoaji wa huduma kwa wananchi.                

                     (iii) Kuboresha utekelezaji wa malengo ya Serikali na kupima matokeo kupitia mfumo       unaokusudiwa kuhakikisha tunapata matokeo makubwa na ya haraka katika maeneo ya kipaumbele na kimkakati katika maendeleo ya Taifa.

Wataalamu watakaojitokeza na kukubaliwa kufanya kazi Serikalini katika maeneo haya, watafanya kazi kwa mikataba ya muda mfupi, lakini inayoweza kuongezwa iwapo utendaji utaridhisha.

Mwito unatolewa kwa Wataalamu wa Kitanzania popote walipo, ughaibuni au ndani ya nchi, kujitokeza na kuleta wasifu wao (CV’s) pamoja na maelezo ya kwa nini wanafikiri wao ni aina ya watu tunaowatafuta. Tumia anuani ifuatayo:-

Katibu Mkuu Kiongozi
Ofisi ya Rais, Ikulu
S.L.P. 9120
DAR ES SALAAM.

Tuesday, November 20, 2012

NORWAY: TANGAZO LA MSIBA

Selyan Samson Ene Sabore

Mtanzania mwenzetu; Selyan Samson Ene Sabore (wa Tøyen, Oslo) amefariki leo jioni nchini Finland alikokuwa kwenye mapumziko na marafiki zake. Selyan alikuwa mazoezini akaanguka na kuzimia kufa (comma) Jumamosi 17 Novemba. Bahati mbaya hakuamka na leo Mwenyezi Mungu ameichukua roho yake. Tunazidi kuwajulisha mipango inavyoendelea. Mwenyezi Mungu Amweke Pema...Ameen!

Celina Mallya akamata Nondoz UKCelina Mallya(wapili toka kulia) akamata nondoz nchini Uingereza pamoja na Watanzania wenzake Mr. Kombo (kushoto) Ruben (wapili toka kushoto) na Mr. Assenga (kulia)
Celina Mallya katika picha ya pamoja na baba mwenye nyumba wake Simbo Mallya
Celina Mallya (kulia) waliosimama) akiwa na Ruben ( Kati waliosimama) wakipata picha ya pamoja na wanafunzi wengine kwenye mahafali ya kukamata nondoz chuoni hapo.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe. Kalage (kati) akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania waliokamata Nondoz kutoka kushoto ni Mr.Kombo, Ruben, Celina na Mr. Assenga

THANKSGIVI​NG SERVICE FOR JOSEPH MANDIA MMBAGO.Thanksgiving service for Joseph Mandia Mmbago will be this
Saturday 24th November 2012
Time: 2:00pm.
Trinity Road Chapel,
Tooting,
London SW17 7HW.
For those of you would like to contribute towards funeral expenses please deposit your money in the following account:
Name:George Siboma.
Sort Code 110001,
Acc No 10332627.
Halifax Bank.

MSIBA NORWAY


A Tanzanian; Selyan Samson Ene Sabore (of Tøyen, Oslo), is no longer with us! Selyan collapsed and fell into a comma during training in Finland on Saturday 17th November. Unfortunately, she died this evening. May Almighty God Rest Her Soul In Peace...Ameen!

TANGAZO LA MSIBA


 
Jesca Emmanuel (12),


Mhe. Tuvako Manongi, Balozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, kwa majonzi makubwa, anasikitika
kutangaza kifo cha Jesca Emmanuel (12), Mtoto wa Afisa mwenzetu Bw.
Emmanuel Swere Alfred na Bi Doto, kilichotokea ghafla siku ya Jumapili
18/11/2012 katika Hospitali ya Mt. Sinai, Queens, New York. Taratibu na
mipango ya kuusafirisha Mwili wa Marehemu Mtoto Jesca kwenda kijijini
Bumbombi- Shirati Tanzania kwa mazishi zinaendelea kwa usimamizi wa
Ubalozi na Familia ya Marehemu.
Taarifa zaidi zitatolewa na Ubalozi kuhusu siku, tarehe na mahali
tutakapomuaga mpendwa wetu Jesca Emmanuel.
Raha ya Milele Umpe Eee Bwana na Mwanga wa Milele Umuangazie
apumzike kwa amani. Amina
UBALOZI WA TANZANIA UMOJA WA MATAIFA
NEW YORK

Thursday, November 15, 2012

KILIO CHA WABONGO WANAFUNZI RUSSIA!!

Wanafunzi Wa Kitanzania Nchini Urusi Wakosa Malazi Na Chakula...!

Sisi wanafunzi wa kitanzania nchini Urusi ,tunakosa huduma za msingi kama vile malazi, chakula na bima ya afya.Serikali kupitia bodi ya mikopo ya elimu ya juu na Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi ,kwania njema iliamua kusomesha wanafunzi wa kitanzania katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Urusi.Lakini kutokana na utendaji mbovu na ubinafsi wa baadhi ya watendaji wa Bodi ya mikopo, kumekua na ucheleweshwaji wa ulipaji wa pesa za kujikimu , malazi na bima ya afya kwa zaidi ya miezi mitatu sasa bila sababu za msingi toka kuanza kwa mwaka wa masomo 2012/13.


Hali hii imetupelekea wanafunzi kuanza kufukuzwa katika hosteli tunazoishi pamoja na kutopatiwa huduma za afya pindi tunapo ugua.Ikumbukwe kuwa katika nchi za ulaya huwezi pata matibabu kama huna bima ya afya.
Shukrani zetu za dhati ziende kwa Ubalozi wa Tanzania nchi Urusi kwa kushirikiana bega kwa bega na Wanafunzi katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili linalotukabili katika kipindi hiki kigumu pamoja na majuku mengi waliyonayo, pamoja na jitihada hizo mpaka sasa hakuna ufumbuzi wowote uliopatikana.
Tunaandika waraka huu kwa huzuni na masikitiko makubwa sana kwa sababu kutopatiwa mikopo mpaka sasa sio tu kunafanya wanafunzi waishi maisha magumu na hatari, vilevile kunatia aibu Taifa kwa kutolipa ada kwa wakati.

Tunaamini kabisa Serikali kupitia bodi ya mikopo ,wizara ya elimu na mafunzo stadi na ufundi na ubalozi wa Tanzania Nchini Urusi una nia njema kabisa kusomesha vijana wake nje ya nchi, ispokua tu kuna baadhi ya watendaji wa bodi ya mikopo wamekua wazembe na kutowajibika kwani wamekua wakitoa majibu ya uongo na jeuri kwa uongozi wa wanafunzi na maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Urusi.

Ombi letu kwenu ni kutufikishia ujumbe huu kwa wahusika na watendaji wa ngazi za juu za bodi ili waweze kutusaidia sisi wanafunzi wa Urusi ambao tupo hatarini huku ugenini.
Tunatumaini kutokana na Uzito wa tatizo letu wahusika watalishughurikia na kulitatua tatizo hili kwa haraka zaidi na kutupa ufafanuzi wa ucheleweshwaji wa mikopo ya wanafunzi kwa zaidi ya miezi mitatu(3).