Umati wa watanzania waishio nchini Italia jana mchana 14 Jan. 2012, walijumuika kwa pamoja mjini napoli kuuaga mwili wa marehemu Twahir Hussein Omari, maarufu kwa wengi kwa jina la utani la "Mboga Zote". Mwili wa marehemu utasafirishwa siku ya Jumanne tokea Rome Fiumicino airport kuelekea Dar-es-salaam na shirika la ndege la KLM na kisha kupelekwa mkoani Tanga kwa mazishi.Mwenyezi Mungu mlaze marehemu mahala pema peponi amen.Picha zaidi zitafuata muda si mrefu.
0 Comments