SHINDANO:
MCH. MWASAPILE (BABU WA LOLIONDO) NA GODBLES LEMA MBUNGE WA ARUSHA MJINI NANI
ZAIDI MWAKA 2011?
Godbles
Lema Mbunge wa Arusha Mjini vs. Mchungaji Mwasapile (Babu wa Loliondo)
Kutokana na maombi ya wengi kutaka kuwashindanisha watu ambao wamefanya mambo ambayo yameigusa jamii ya kitanzania kwa mwaka wa 2011 Blog yenu kwa mtazamo wa haraka kwa mwaka huu imeona iwashindanishe Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbles Lema na Mch. Mwasapile (Babu wa Loliondo).
Blog yenu baada ya kuwaingiza hao kwenye kinyang'anyiro hicho inapenda kuwaelezea kila mmoja kwa kifupi ni kwa nini ameingia.
Tukianzia na Mh. Lema ni Mbunge
kijana ambaye amekutana na mikiki mingi ya kisiasa ukizingatia yeye ni mara
yake ya kwanza kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameweza
kupambana na majaribu mbali mbali ya kisiasa mpaka kumpelekea kugoma kupata
dhamana ya kesi mojawapo katika kesi zinazomkabili na kuamua kwenda rumande ili
ujumbe wake ufike, na vile vile kutokana na kura ambazo zilikuwa zinapigwa
kutoka Blog ya Mjengwa akishindanishwa na wanasiasa mbali mbali ambao wengi wao
ni vijana wenzie nakuweza kushinda katika kinyang'anyiro hicho.
Tukirudi kwa Mch. Mwasapile almaarufu kama Babu wa Loliondo au Babu Ambi, yeye ameingia kwenye kinyang'anyiro hiki kutokana na yeye kuwateka watanzania watoto, vijana na wazee katika nafasi zao mbali mbali kwa staili yake ya kugawa tiba ya asili kwa kutumia kikombe maarufu kama kikombe cha babu.
Mchungaji huyu alianza kutoa huduma hii mwanzoni mwa mwaka huu na kujizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania kutokana na watu wengi kuamini dawa anayotoa kwa kutumia kikombe hicho inatibu magonjwa yote sugu yakiwemo Ukimwi, kisukari, TB na mengine mengi, kutokana na tukio hili kuwahusisha watu mbali mbali, ata wale wenye nyadhifa za juu tumeona Babu huyu anafaa kuingia kwenye mtanange huu.
TAFADHALI PIGA KURA YAKO KWA KUTUMIA UJUMBE WA MAANDISHI KWENDA NAMBA +255 714945143
UKIWA KWENYE ENEO LA KUANDIKA UJUMBE KWENYE SIMU YAKO UTAANDIKA:
"2011 WINNER
BABU" AU
"2011 WINNER
LEMA"
TUMA KWENYE NAMBA HIYO HAPO JUU, MWISHO SAA
5.59 USIKU WA TAREHE. 31-12-2011.
MAJIBU YATATOLEWA TAR. 01-01-2012
0 Comments