Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

JAPAN:MKUSANYIKO WA WATANZANIA KWA TAFRIJA FUPI YA KIPINDI HIKI CHA SUMMER.

KWA WATANZANIA JAPAN:
Nadhani baadhi yenu mnayo taarifa. Kwa wale ambao hawajapata taarifa, ningependa kuwaarifu kuwa Jumamosi hii, tarehe 13/Aug/2011, kutakuwa na mkusanyiko wa watanzania wote huko maeneo ya Sagamino. Mkusanyiko huu utafanyika kando ya mto (ni kama beach), na kutakuwa na vinywaji, chakula na nyama za kuchoma na muziki. Maandalizi yameshafikia hatua kubwa.
Kiingilio ni Yen 3,000. Wale ambao hawajachanga wanaweza kuchanga kupitia akaunti ya jumuiya ambayo ni hii hapa chini. Mwisho wa kuchanga ni Alhamisi ya wiki hii (Tar 11/ Aug/2011).
Benki: Sumitomo Mitsui Banking Corporation
Tawi: Kunitachi: No. 666
Jina la Akaunti: Tanzanite Society; Msimamizi: Njenga Rashid Omar
Account No. 7916169

Shughuli hii itaanza rasmi saa 6 asubuhi na kuendelea hadi saa 12 jioni. Na kwa wale watakaopenda kuendelea baada ya hapo huenda wakaruhusiwa. Mkusanyiko huu siyo rasmi kwa hiyo hatutakuwa na hotuba zozote mbali na miongozo itakayotolewa pale inapohitajika.
Lengo ni kukusanyika watanzania wote na marafiki zetu wa karibu kujumuika pamoja na kufahamiana, kuongea na kubadilishana mawazo. Mkusanyiko huu umeandaliwa na wenzetu wa Sagamino na Jumuiya yetu Tanzanite, imeuunga mkono kwa kuwa ni moja ya sera zetu ni kuwaweka watanzania wote wanaoishi hapa Japan kuwa pamoja na kuwa na umoja ulioimarika.
Mkuusanyiko huu ni wa watanzania wote bila kutenga wanachama na wasio wanachama wa Tanzanite. Kutakuwa na kitabu cha kujiandikisha kwa wale wataoona wako tayari kujiunga na kutakuwa na kitabu cha kukusanya michango yetu ya mwezi. Malipo haya pia unaweza kulipa moja kwa moja kwenye akaunti yetu na kutujulisha kwa barua pepe.
Kama muda unaruhusu tafadhali usisite kujumuika nasi. Tunasikitika hatukuweza kuandaa utaratibu maalum kwa wenzetu ambao wapo kwenye mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, lakini kama watapenda kuja kujumuika kwa ajili ya kukutana na kufahamiana, wanakaribishwa.
STESHENI YA KARIBU NI SOBUDAEMAE (ODAKYU LINE) Ukifika stesheni piga simu zifuatazo na utapewa maelekezo zaidi. Mkusanyiko huu unafanyika kando ya mto, bahati mbaya hatuna address kwa wale ambao wangependa kutumia navigation za magari yao kuwafikisha hapo. Ukifika na gari mpaka stesheni hii pia tutakuelekeza.
1. Gwakisa : 080-3242-7442
2. Njenga : 090-6305-6041
3. Mwombeki : 080-2258-7587
4. Kidume : 080-3150-9173
5. Pembe : 080-3458-8786

NJENGA, Rashid
Mwenyekiti
Tanzanite Society, Japan

Post a Comment

0 Comments