Baadhi ya Watanzania pichani wakisubiri kumsalia marehemu
Kwa uwezo wa Allah na ushirikiano wa hali ya juu uliopo kati yetu (watanzania wa ugiriki) tumeweza kufanikisha mchango wa kumsafirisha mwenzetu SAIDI HASSAN MGOI (Maarufu kwa jina la CHANCE) ili akazikwe nyumbani. Mwili wa Marehemu utawasili Dar J'mosi13/08 saa NANE NA NUSU USIKU kwa ndege ya shirika la Uturuki.
Marehemu alikoshwa,alikafiniwa na kuswaliwa katika msikiti wa ELSALAAM uliopo Neos Kosmos Athens.Idadi kubwa ya watanzania walihudhuria msikitini.
Taarifa tulizo nazo khs maziko yatafanyika J'pili 14/8 saa saba mchana Tandika Mikoroshini kwa SANDARI ila kwa maelezo kirefu fanyeni mawasiliano na FATUMA dada yake (0718567537) au (0783694736)
Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi Amin.Taarifa tulizo nazo khs maziko yatafanyika J'pili 14/8 saa saba mchana Tandika Mikoroshini kwa SANDARI ila kwa maelezo kirefu fanyeni mawasiliano na FATUMA dada yake (0718567537) au (0783694736)
INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUUN
Kayu Ligopora
KATIBU wa JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI
1 Comments