Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Dhibiti Mlipuko: COVID-19 Tanzania

https://www.gofundme.com/f/dhibiti-mlipuko-covid19-tanzania
Dhibiti Mlipuko: COVID-19 Tanzania

Mlipuko wa Corona unatishia usalama wa maisha ya Wataanzania walio wengi. Bila tahadhari ya haraka na ya kutosha, wengi wanaweza kupata maambukizi, na hata kupoteza maisha yao. Tunahitaji kushirikiana kwa haraka, pamoja na ndugu zetu nyumbani, kupigana  na vita hii.

Kama mtanzania uishio nje ya Tanzania (Diaspora), tunaomba mchango wako wa kifedha kufanikisha jitihada za kudhibiti mlipuko wa COVID-19 nyumbani. Kampeni hii ya “Dhibiti Mlipuko: COVID-19 Tanzania” ni kampeni inayohusisha ushirikiano wa taasisi na jumuiya za watanzania kwenye majimbo mbalimbali ya marekani.

 Njia za Utumaji wa Michango: Pamoja na GoFundMe, unaweza kuwakilisha mchango wako kupitia CashApp ($TZDiaspora au namba ya simu 612 229 2919 ).

 Tarehe ya mwisho ya kuwakilisha michango ni 30 Aprili, 2020

 Tafadhali zingatia yafuatayo:

1.  Kama unatumia CashApp au Zelle, tafadhali tunaomba bofya hapa (TAARIFA YA MCHANGIAJI  ) ututumie jina lako, anuani ya barua pepe na namba ya simu, ili tukutumie barua kwa ajili ya punguzo la kodi (tax return).

2.  Kama unatumia Zelle kutuma mchango, unahitaji  kufuata maelezo hapa - ZELLE . Kama unatuma mchango wako kupitia benki, tafadhali pata taarifa za benki kupitia hapa – BANK WIRE INFORMATION .

3.   Barua zitatolewa kwa wale tu waliochangia kiwango cha kuanzia US$250, kufuatana na kanuni za US Internal Revenue Service.

4.    Kampeni hii inaratibiwa na kamati ya watanzania wachache waliojitolea, ikishauriwa na viongozi wa jumuiya na taasisi. Uhasibu wa michango unasisimamiwa na taasisi ya DICOTA .

5.      Usimamizi wa utoaji wa msaada kutoka kwenye michango utafanyika kwa ushirikiano na viongozi wa jumuiya, na ripoti ya uhasibu itatolewa kwa wachangiaji baada ya zoezi zima kuisha.


Aidha, tunakusihi ujikinge na uwakinge wenzako: Kaa nyumbani, Osha mikono, Tumia barakoa, na Epuka mikusanyiko.

Umoja wetu, ndio nguvu yetu.

 Asanteni!
N.B: Wasiliana nasi kwa barua pepe -- dhibiticovidtz@gmail.com

Post a Comment

0 Comments