Taswira Mbalimbali Za Mkutano W a Watanzania Waishio Nchini Australia na Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mwenyekiti wa watanzania waishio Australia Asimwe Kabunga katika mkutano unaowajumuisha watanzania waishio Australia okt,26-2011. Rais Jakaya Kikwete pamoja wanajumuia ya watanzania wanaoishi Australia wamezungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo,
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete(kulia) akipokea maua kutoka kwa mweka Hazina wa Jumuia ya Watanzania waishio Australia Maryam Powell (oktober 26,2011) walipokutana na wanajumia mjini Perth Australia .Rais Jakaya Kikwete alikutana na wanajumuia kuzungumza mambo mbalimbali ya maendeleo na kijamii, Rais yupo nchini Perth Australia kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuia ya madola( commonwealth Heads of Government meeting- CHOGM 2011,utakaanza Oktober 28-30,2011, -
Mama Salma Kikwete akisalimiana na mmoja wa wanajumuia.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akibadilisha mawazo na mwanajumuia wa Australia Dr.Joseph Masika wakati Rais Jakaya Kikwete alipokutana na wanajumuia wanaoishi Australia 0ktoba 26,2011 . na kuzungumza nao mambo mbalimbali ya maendeleo ya nchi yetu
Baadhi ya wanajumuia wanaoishi nchini Australia wakimsikiliza. Rais Jakaya Kikwete hayupo pichani alipokutana nao Okt.26.2011.
Baadhi ya wanajumuia wanaoishi nchini Australia wakimsikiliza. Rais Jakaya Kikwete hayupo pichani alipokutana nao Okt.26.2011. nchini Perth
Picha ya pamoja ya wanajumuia wa kike wanaoishi Australia pamoja na Mke wa Rais na Mama Salma Kikwete baada ya kuamlizika mkutano wa Rais Kikwete na Watanzania wanaoishi Australia,(okt,26,2011).Picha na Mwanakombo Juma-MAELEZO
0 Comments