MAONI
YANGU KUHUSU
MABADILIKO YA KATIBA
Nadhani ingependeza kama nasi huku ughaibuni tungekuwa tunabadilishana mawazo kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya katiba(INGAWA KUNA WALE WANAOAMINI KUWA HATUNA TUNACHOWEZA KUBADILISHA.KILA KITU KIMESHAAMULIWA NA WAKUU WENYE SAUTI TANZANIA).
Mimi nilishayapeleka yangu www.katiba.go.tz.Na kama wengi wetu hawana wakati wa kueleza mengi , ni bora tujaze hili suala la URAIA PACHA Bila ya sisi huku ughaibuni kulipigia debe, huenda na wale wa nyumbani hata wasilikumbuke.
Maoni
yangu yana sehemu nne kuu zifuatazo:
1.
KINGA YA RAISI .
Anapokuwa
madarakani asishtakiwe ila mara tu muhula wake wa kuongoza
unapokwisha na siku anapoapishwa Raisi mpya,KINGA ya Raisi mstaafu
ifutike automatically ili aweze kushtakiwa kwa makosa aliyoyafanya
katika kipindi cha uongozi wake.Na ikipita miaka mitano tangu
kumaliza uongozi na akawa hakushtakiwa kwa kosa lolote ,Kinga yake
arudishiwe na kuanzia hapo hatoweza tena kushtakiwa.
(UCHAMBUZI
)Viongozi wengi wa Afrika wanatumia vibaya mno madaraka yao
wakijijua kuwa hawatoshtakiwa wanapotoka madarakani.Kuwepo kipengee
hiki kutasaidia wapunguze ubadhirifu wanapokuwa madarakani.
2.
WAFUNGWA:
a)
HUKUMU YA KIFO ISIWEPO. Kwa kosa lolote HATA LA KUUA
AU LA UHAINI.Hukumu ya juu iwe ni kifungo cha maisha.
(UCHAMBUZI
)Tunapomuua tunakuwa tumempumzisha na wala hatohisi uchungu wa
adhabu kwa lile kosa alilofanya.Mimi hapa wala silalii katika ile
hoja ya HAKI YA MWANADAMU KUISHI wanayoitumia baadhi ya wale
wanaopinga hukumu ya kifo duniani.
b)KITUMIKE
KIFUNGO CHA NJE NA KAZI ZA KUNUFAISHA JAMII kwa makosa
yasiyokuwa ya jinai,
(UCHAMBUZI
) Ndugu zetu wengi hupelekwa rumande kwa kuiba kuku na wanapotakiwa
watoe dhamana wanashindwa na hurundikwa rumande na nchi hulazimika
kuwahudumia bila faida yoyote.Kinachosikitisha wengi wanaokwenda
rumande ni hawa ndugu zetu masikini wakati wale wenye uwezo wa
kiuchumi (na hasa wageni)hulipa kiwango chochote wanachotakiwa na
wanakuwa na uhakika wa kutokwenda jela.!!
c)IFUTWE
CRIMINAL RECORD baada ya kupita miaka kumi tangu
mfungwa kumaliza kifungo chake bila kufanya kosa jingine
la jinai.
(UCHAMBUZI)
Wafungwa wanapomaliza kifungo huwa wanabaki maisha yao yote katika
records za INTERPOL kuwa ni criminals, na
hii inawakosesha haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi katika
jamii yao au hata kupata kazi kwa kuwa huonekana ni criminals.Hali
hii inawafanya wengi warudie tena katika uharamia kwa sababu
wanajihisi kuwa jamii haiwapi nafasi ya kubadilisha au kuifuta sifa
mbaya ya u -crimial inayowaandama maisha
yao yote kutokana na justice system ilivyo ya kidhuluma na uonevu
duniani.
3.
MUUNGANO:
Kuwe
na nchi inayoitwa ZANZIBAR ,
Kuwe
na nchi inayoitwa TANGANYIKA (au jina lolote litalochaguliwa)
Kuwe
na mfumo wa Muungano utaokubalika na pande zote
mbili( Kazi hii tuwachie wataalamu siyo kila mtu anaiweza).
4.
URAIA PACHA(DUAL CITIZENSHIP)
Raia
waruhusiwe kuwa na uraia pacha
(UCHAMBUZI)
Hapa sina haja ya kuchambua kwa sababu zinaeleweka wazi faida za
uraia pacha na mifano ipo wazi kwa zile nchi zenye mfumo huu jinsi
zinavyofaidika katika kila nyanja.HAKUNA
hasara wala madhara ya kuwa na uraia pacha zaidi ya faida tu.
KAYU
LIGOPORA
ATHENS
0 Comments