JE
HATI YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR IPO AU HAIPO?
Katika
elimu ya Mantiki kuna kanuni nyepesi za kuufikia ukweli,kuna kanuni
nyepesi zinazoweza kumuongoza mtu kuelewa kirahisi ukweli ulipo na
hasa kama kuna maelezo ya pande mbili zinazogongana. Lakini katika
siasa HAKUNA KABISA KANUNI ZA KUUJUA UKWELI. Kwenye siasa maslahi na
MACHIAVELLISM(End
justifies the means) hutumika
sana bila hata kumwogopa Mungu!!!!!Wakati mwingine viongozi wa siasa
-ambao hujisahau na kujiona wana akili nyingi na busara kuliko wale
wanaowaongoza- hufanya mambo ambayo hata mtoto wa miaka miwili
hugundua wazi kuwa KUNA KASORO KATIKA MAELEZO WANAYOYATOA!!!
Utangulizi
wa hapo juu unanifikisha moja kwa moja katika kulichambua jibu la
swali tunalojiuliza wengi JE HATI YA MUUNGANO IPO?
“RAIS
SHEIN” anasema IPO(anaetaka anaweza kuiona UN.)
“RAIS
MSTAAFU KARUME” anasema HAJAWAHI KUIONA(Hakuwahi kuiona katika
kipindi chote alipokuwa Rais)
Kwa
wale waliozowea kuchezea maneno watahoji kuwa “KUTOIONA”does not
necessarily mean kwamba “HAIPO”- Lakini inajionesha wazi kuwa
anamaanisha “HAIPO”.
Kwa
hiyo tuna viongozi wakuu wawili wenye maelezo yanayogongana:
“A”
anasema HATI YA MUUNGANO IPO.
“B”anasema
HATI YA MUUNGANO HAIPO
Je
ukweli upo wapi kati ya maelezo ya “A” na ya “B?
Cha
kusikitisha ni kuwa katika hatua za kuutafuta utatuzi, siyo tu
kuhusiana na Hati ya Muungano bali hata katika kujadili suala la
mfumo gani wa Muungano uwepo kati ya Wazanzibari na Watanzania bara)
mara nyingi watu tumekuwa tukitumia sana emotion,michemko,hasira,to
the extent watu kujihisi kama sisi ni pande mbili za maadui!!!!WAKATI
KIUKWELI SISI NI PANDE MBILI ZA WANANDUGU.(Ukisoma rai zinazotolewa
mitandaoni toka kwa wale wenye misimamo mikali wa pande zote mbili
za Bara na Visiwani hutochelewa kuona wazi maelezo yanayovuka mipaka)
Kabla
sijakamilisha maelezo yangu nina furaha kubwa kuyanukuu maelezo
mazuri na ya busara yaliyoandikwa na Ashakh Kiongozi
(Mzalendo.net)02/02/2013 11:07 alipokuwa akitoa ushauri wa jinsi gani
ya kulipata jibu la Hati ya Muungano.Na hapa namnukuu :
“Tukumbuke
hata mahkama chini ya mwanasheria mkuu wa Zanzibar wakati huo Bw Iddi
Pandu Hassan alithibitisha kwamba hajawahi kuuona na Serikali ya
Zanzibar haina mkataba huo.
Naamini Dr Shein
kasema kwa maana yake kuwa mkataba wanao. Sasa ni jukumu letu la
kumwambia atuonyeshe na sie hapahapa Zanzibar bila ya kwenda NewYork.
Tutumie Njia za busara za kumwambia atuonyeshe, kama hivi:
1) Maalim Seif – yeye ni makamo athibitishe ukweli huu hasa kwa vile anakwenda na kuingia Ikulu.
2) Mh Aboubakar – Waziri wa Sheria athibitishe kwa mujibu wa sheria mkataba huu ulipo.
3) Othman Masoud – Mwanasheria yeye ndie nundu wa hili
4) Jaji OMar Makungu – Jaji Mkuu wa Zanzibar kisheria tayari wameshatoa maamuzi yao
5) Makachero – ni ukifika wakati ni lazima makachero wafanye kazi yao ili kutupa japo copy yake
Hii
ni mbiu ya mgambo kutoka kwa Dr Shein, huu ndio mwanya mzuri wa
kuuona mkataba wetu ikiwa tunao na upo.”
Mwisho wa kumnukuu
Namalizia
kwa kusema:
Mimi
niandikaye maelezo haya natoka TANZANIA BARA . nimejitahidi na
naendelea kujitahidi kutotumia michemko wala hasira katika kuielezea
hali ya MUSTAKBAL WA MUUNGANO WETU ambao kwa kiasi kikubwa naamini
vyovyote utakavyokuwa uamuzi wa maoni ya katiba mpya,(uwe wa mkataba
uwe wa serikali 3 au 1) uamuzi huo HAUTOUFUTA UDUGU ULIOPO KATI
YETU. Na hata kama kutakuwepo na wenye misimamo mikali toka pande
zote mbili, watu hao hawatofanikiwa kupandikiza chuki katika nyoyo
za wengi wanaopenda kusiwe na chuki kati yetu.
Nafunga
maelezo yangu kwa kuwaomba wote tunaoishi ughaibuni TUSIATHIRIKE na
michemko ya nyumbani tukawa tunaihamishia huku bila kuzingatia
mazingira halisi ya mfumo wa maisha yetu ya huku.Mazingira ya huku
yanahitaji zaidi mshikamano ,busara utulivu na kuvumiliana bila
kujali wapi anatoka kila mmoja wetu.TUSICHANGANYE MAMBO TUTAKUJA
VURUGA.
Namuomba
Mola atulinde na atuzidishie hekima (Amin.)
KAYU
LIGOPORA
ATHENS
GREECE.
kaygreko@yahoo.com
0 Comments