Marehemu Twahir hussein Omari maarufu kwa jina la Kaka Twaa au Mboga zote
JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MTANZANIA PICHANI NDUGU TWAHIR HUSSEIN OMARI KILICHOTEKEA JANA USIKU MJINI NAPOLI. SABABU YA KIFO CHAKE ITAPATIKANA BAADAE BAADA YA UCHUNGUZI WA MADAKTARI. MIPANGO YA MAZISHI TAYARI INAFANYWA JUMUIYA INAWATAKA WATANZANIA KUJITOKEZA KWA WINGI NA KUJITOLEA ZAIDI KATIKA MICHANGO ILI KUWEZA KUUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU NYUMBANI. MAREHEMU NI MWENYEJI WA TANGA BARABARA 15.NA HAPA ITALY ALIKUWA AKIISHI MJINI MODENA. MATAWI YOTE YA JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA NA JUMUIYA ZOTE ZINAOMBWA KUKUTANA MARA MOJA ILI KUKUSANYA MICHANGO. KWA MAWASILIANO WASILIANA NA KATIBU N° +39 329 4149 712
TUNAUNGANA NA WATANZANIA WOTE WANAOMFAHAMU , NDUGU NA WAZAZI KATIKA WAKATI HUU MGUMU WA MAOMBOLEZO. MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA! AMIN!
0 Comments