Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

WASHINGTON D.C: MSIBA !!!





Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeitwa Steina Mrema ambaye alikuwa ni mkazi wa jimbo la Pennslyvania nchini Marekani amefariki dunia siku ya tarehe 21/12/2011 mjini Washington, D.C.

Mipango ya kuusafirisha mwili wa marehemu Steina Mrema kurudishwa nyumbani Tanzania bado inaendelea katika miji ya Washington D.C na College Park, Pennslyvania.

Watanzania kutoka sehemu mbalimbali duniani mnaombwa kusaidia kuchangia gharama za kufanikisha kumrudisha marehemu nyumbani Tanzania.

Mpaka hivi sasa bado zinahitajika zaidi ya $6000 ili kuwezesha kumsafirisha marehemu ili akampumzike milele.

Kwa wale wakazi wa Washington, DC, Maryland na Virginia mnaombwa na kukaribishwa kuendelea kutoa michango yenu, michango hiyo iwasilishwe nyumbani kwa Rashid Mkakile katika anuani ya 9005 Locust Spring Dr, College Park, MD 20740.

Kwa wengine walio mbali, imefunguliwa akaunti maalum kwa ajili ya kuwasilisha michango kwa ajili ya huu msiba.

Maelezo ya akaunti hiyo ni: Elimchile Lyaro, Wells Fargo Bank, Account #7015276038 na Routing # 055003201.

Kwa wakazi wa Pennslyvania msiba huu upo nyumbani kwa Elimchile Lyaro katika anuani ya 626 Bridge Street, College, PA 19426.

Msiba huu ni wa Watanzania wote ndugu, jamaa na marafiki. Umoja, mshikamano na ushirikiano ndio utakaowezesha na hatimae kufanikisha kuusafirisha mwili wa marehemu nyumbani Tanzania kwenye mapumziko ya milele.


Post a Comment

0 Comments