Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkazi wa mji wa Lansing katika jimbo la Michigan nchini Marekani anaeitwa Nasibu Juma Manyala amefariki dunia.
Mtanzania huyo alifariki dunia siku ya tarehe 22/10/2011 katika mji wa Lansing, Michigan nchini Marekani. Marehemu ambaye amecha mtoto mmoja anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne tarehe 22/11/2011 saa sita mchana mjini Lansing, MI, USA.
Maandalizi ya mazishi bado yanaendelea na familia ya marehemu inaomba msaada wako ili iweze kukidhi gharama za kufanikisha mazishi hayo na kumpumzisha marehemu milele.
Marafiki na watanzania wengine wote walio karibu na mji wa Lansing mnaombwa kuhudhuria kwa wingi na kusaidia kwa hali na mali ili kufanikisha msiba huu.
Anuani ya eneo la shughuli za mazishi ni ifuatayo;
12 Noon
Estes-Ladley
325 W. Washtenaw St.
Lansing, MI 48842
Kwa wale wote ambao watapenda kuchangia, tafadhali tuma mchango wako moja kwa moja kwenye akaunti ifuatayo;
Nasibu J. Manyala Memorial Account
MSU Federal Credit Union
Account # 43380705
Routing# 272479663
Pia habari zaidi unaweza kuwasiliana na watu wafuatao;
Deo Ngonyani kupitia simu #
David Adam Mssika
Musa Maingu
Bushiri Abdallah
Siz Karlo
0 Comments