MKUTANO WA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA UHURU WA TANZANIA BARA NCHINI ITALY
2:45 PM
Kaimu balozi wa ubalozi wa Tanzania Italy, Mh. Salvator Mbilinyi, anapenda kuwafahamisha viongozi wa Jumuiya zote za Watanzania nchini Italy kuwa, ijumaa tarehe 25 Nov. 2011, kutakuwa na mkutano wa maandalizi ya sherehe za uhuru wa Tanzania bara. Mkutano utafanyika kuanzia saa nne asubuhi kwenye ubalozi wa Tanzania Italy, mjini Rome,Via Cortina d'ampezzo 185. Viongozi mnaombwa mfike maana muda wa maandalizi ni mdogo.
NB:Mkutano huu ni kwa viongozi au wawakilishi wao tu na si kila mtu.
0 Comments