Mtandao wa WABONGO UGHAIBUNI KWA niaba ya WATANZANIA WOTE UGHAIBUNI imezipokea taarifa za ajali kwa masikitiko makubwa tunachukua nafasi hii kuungana na Ndugu na jamaa pamoja na Taifa zima kuwa tuko pamoja katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.Mwenyezi Mungu aziweke roho zao peponi. Kwa wale waliookoka,tunamuomba Mola awakutanishe na familia zao wakiwa katika hali ya afya,utulivu na usalama.
Ni matumaini yetu vyombo husika vitatoa maelezo kamili kuhusiana na ajali ili ziweze kuchukuliwa taadhari zaidi siku za usoni.
(Tembelea WABONGO UGHAIBUNI )
MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!!
0 Comments