Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

UZAMAJI WA MELI YA MV SPICE ISLANDERS

UZAMAJI WA MELI YA MV SPICE ISLANDERS

1. Jumuiya ya watanzania ugiriki inachukua nafasi hii kutoa pole na kuelezea masikitiko na huzuni za watanzania wote wa hapa kwa ndugu na jamaa wa marehemu.Mwenyezi Mungu aziweke roho zao peponi.
2.
Kwa wale waliookoka,tunamuomba Mola awakutanishe na familia zao wakiwa katika hali ya afya,utulivu na usalama.
3.
Katika mkutano wa wanajumuiya (tuliokuwa tumeshaupanga kufanyika leo 10/09/2011) tutawakumbuka kwa dua wale wote waliofariki na wale wote waliookoka katika ajali hii.
4.
Tunaamini viongozi wetu wana uwezo mkubwa na wa hali ya juu wa kufuatilia na kujua sababu halisi za ajali na kuhakikisha ajali kama hii haitokei kirahisi katika siku za usoni.

Kayu Ligopora
Katibu wa jumuiya

Post a Comment

0 Comments