Blogger Widgets

Newdeal Africa

Tuesday, February 5, 2013

JE HATI YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR IPO?JE HATI YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR IPO AU HAIPO?

Katika elimu ya Mantiki kuna kanuni nyepesi za kuufikia ukweli,kuna kanuni nyepesi zinazoweza kumuongoza mtu kuelewa kirahisi ukweli ulipo na hasa kama kuna maelezo ya pande mbili zinazogongana. Lakini katika siasa HAKUNA KABISA KANUNI ZA KUUJUA UKWELI. Kwenye siasa maslahi na MACHIAVELLISM(End justifies the means) hutumika sana bila hata kumwogopa Mungu!!!!!Wakati mwingine viongozi wa siasa -ambao hujisahau na kujiona wana akili nyingi na busara kuliko wale wanaowaongoza- hufanya mambo ambayo hata mtoto wa miaka miwili hugundua wazi kuwa KUNA KASORO KATIKA MAELEZO WANAYOYATOA!!!
Utangulizi wa hapo juu unanifikisha moja kwa moja katika kulichambua jibu la swali tunalojiuliza wengi JE HATI YA MUUNGANO IPO?
RAIS SHEIN” anasema IPO(anaetaka anaweza kuiona UN.)
RAIS MSTAAFU KARUME” anasema HAJAWAHI KUIONA(Hakuwahi kuiona katika kipindi chote alipokuwa Rais)
Kwa wale waliozowea kuchezea maneno watahoji kuwa “KUTOIONA”does not necessarily mean kwamba “HAIPO”- Lakini inajionesha wazi kuwa anamaanisha “HAIPO”.
Kwa hiyo tuna viongozi wakuu wawili wenye maelezo yanayogongana:
A” anasema HATI YA MUUNGANO IPO.
B”anasema HATI YA MUUNGANO HAIPO
Je ukweli upo wapi kati ya maelezo ya “A” na ya “B?
Cha kusikitisha ni kuwa katika hatua za kuutafuta utatuzi, siyo tu kuhusiana na Hati ya Muungano bali hata katika kujadili suala la mfumo gani wa Muungano uwepo kati ya Wazanzibari na Watanzania bara) mara nyingi watu tumekuwa tukitumia sana emotion,michemko,hasira,to the extent watu kujihisi kama sisi ni pande mbili za maadui!!!!WAKATI KIUKWELI SISI NI PANDE MBILI ZA WANANDUGU.(Ukisoma rai zinazotolewa mitandaoni toka kwa wale wenye misimamo mikali wa pande zote mbili za Bara na Visiwani hutochelewa kuona wazi maelezo yanayovuka mipaka)


Kabla sijakamilisha maelezo yangu nina furaha kubwa kuyanukuu maelezo mazuri na ya busara yaliyoandikwa na Ashakh Kiongozi (Mzalendo.net)02/02/2013 11:07 alipokuwa akitoa ushauri wa jinsi gani ya kulipata jibu la Hati ya Muungano.Na hapa namnukuu :
Tukumbuke hata mahkama chini ya mwanasheria mkuu wa Zanzibar wakati huo Bw Iddi Pandu Hassan alithibitisha kwamba hajawahi kuuona na Serikali ya Zanzibar haina mkataba huo.
Naamini Dr Shein kasema kwa maana yake kuwa mkataba wanao. Sasa ni jukumu letu la kumwambia atuonyeshe na sie hapahapa Zanzibar bila ya kwenda NewYork.
Tutumie Njia za busara za kumwambia atuonyeshe, kama hivi:
1) Maalim Seif – yeye ni makamo athibitishe ukweli huu hasa kwa vile anakwenda na kuingia Ikulu.
2) Mh Aboubakar – Waziri wa Sheria athibitishe kwa mujibu wa sheria mkataba huu ulipo.
3) Othman Masoud – Mwanasheria yeye ndie nundu wa hili
4) Jaji OMar Makungu – Jaji Mkuu wa Zanzibar kisheria tayari wameshatoa maamuzi yao
5) Makachero – ni ukifika wakati ni lazima makachero wafanye kazi yao ili kutupa japo copy yake

Hii ni mbiu ya mgambo kutoka kwa Dr Shein, huu ndio mwanya mzuri wa kuuona mkataba wetu ikiwa tunao na upo.” Mwisho wa kumnukuu
Namalizia kwa kusema:
Mimi niandikaye maelezo haya natoka TANZANIA BARA . nimejitahidi na naendelea kujitahidi kutotumia michemko wala hasira katika kuielezea hali ya MUSTAKBAL WA MUUNGANO WETU ambao kwa kiasi kikubwa naamini vyovyote utakavyokuwa uamuzi wa maoni ya katiba mpya,(uwe wa mkataba uwe wa serikali 3 au 1) uamuzi huo HAUTOUFUTA UDUGU ULIOPO KATI YETU. Na hata kama kutakuwepo na wenye misimamo mikali toka pande zote mbili, watu hao hawatofanikiwa kupandikiza chuki katika nyoyo za wengi wanaopenda kusiwe na chuki kati yetu.
Nafunga maelezo yangu kwa kuwaomba wote tunaoishi ughaibuni TUSIATHIRIKE na michemko ya nyumbani tukawa tunaihamishia huku bila kuzingatia mazingira halisi ya mfumo wa maisha yetu ya huku.Mazingira ya huku yanahitaji zaidi mshikamano ,busara utulivu na kuvumiliana bila kujali wapi anatoka kila mmoja wetu.TUSICHANGANYE MAMBO TUTAKUJA VURUGA.
Namuomba Mola atulinde na atuzidishie hekima (Amin.)
                                                                                                   KAYU LIGOPORA
ATHENS GREECE.
kaygreko@yahoo.com  

0 comments: