TUANZIE WAPI?
Lengo kuu la maandishi yangu siyo kutaka kubadilisha
mambo,bali napenda kusikiliza rai tofauti
na marekebisho toka kwa ndugu na marafiki wataosoma uchambuzi wangu
ambao ulikuwa umenikaa kooni muda mrefu na nilikuwa natafuta nafasi ya kuumwaga
hadharani kwa wenzangu wenye mtazamo mzuri zaidi waweze kunisahihisha ili nami
nizinduke.
Baada ya kuangalia kwa utulivu jinsi maamuzi na mabadiliko
yanavyofikiwa katika nchi zetu za kiafrika na sehemu nyingi duniani , nimefikia
kukinaika ,kuna makundi matatu makuu yanayotuongoza au yanayotusukuma kufikia
maamuzi fulani. Na kila kundi lina sifa na nguvu za kuathiri zinazotofautiana
na kundi jingine. SIZUNGUMZII
INDIVIDUALS WALIOMO NDANI YA MAKUNDI HAYO BALI NAZUNGUMZIA MAKUNDI AS MECHANISM.
Kundi la kwanza :WANASIASA
Kundi la pili:MATAJIRI
WAKUBWA(Siyo wajasiriamali wala wanauchumi)
Kundi la tatu: VIONGOZI
WA DINI. Siyo dini ni “VIONGOZI WA DINI” yoyote anayoiamini kila
mmoja wetu.
Kila kundi lina sifa na mfumo tofauti na jingine . Kati ya
kundi la kwanza na la pili kuna
kijikundi kina nguvu za ajabu, kikundi hiki ni cha “USALAMA NA UPELELEZI”. Aidha
kuna kijikundi kingine cha WACHUNGA MASLAHI”. Wahusika wa kikundi hiki
hujihusisha na kujiingiza katika makundi yote matatu kulingana na hali ya
maslahi itavyowavuta. Kijikundi hiki ni hatari mno, hakina simile katika
kuhakikisha wanafanikisha kile wakitakacho au kile walichotakiwa wakifanye ili
mradi lengo likamilike.Tofauti muhimu iliyopo kati ya kijikundi hiki na wale
MATAJIRI WAKUBWA ni kuwa wahusika wa kijikundi hiki HUJIFICHA na huonekana tu matunda ya vitendo
vyao.Wachache hujulikana baada ya mibiginyo inayofanywa ili pia kulinda maslahi
makuu.
NB. Sikutaja kundi la WANAJESHI ambao kila demokrasia
inavyozidi kukua Afrika wanajikuta ni kundi la kutekeleza maamuzi ya wanasiasa -
hata kama hawakubaliani nayo-(WITH EXCEPTION OF EGYPT RECENTLY) tofauti na miaka ya nyuma walipokuwa wakifanya mapinduzi ya mara kwa
mara. Aidha sikutaja vyombo vya habari ambavyo vyote vipo chini ya MATAJIRI WAKUBWA
au WANASIASA . Ama wale wanaojiita wanablogs wao nawaweka katika kundi la “WACHUNGA
MASLAHI” kwani ni wachache mno kati yao wanaoelezea fikra zao huru.
Kundi la kwanza : WANASIASA.
Sifa kuu za kundi hili ni: UONGO NA KUBADILISHA MISIMAMO
Hakuna kiongozi yeyote duniani aliyetekeleza kikamilifu yale
yote aliyoyaahidi kabla ya kuchaguliwa kuwa kiongozi.Ajabu ya mambo sisi
waongozwa kila siku tunawataka wawe wakweli na wasibadili misimamo!!!Nadhani
kuna sababu ya wazi inayowalazimu wajivishe sifa hii, sababu ambayo sisi
waongozwa daima haitugusi katika maisha yetu ya kila siku,Sababu hiyo ni kuwa
wanapoingia madarakani hukumbana na mibiginyo na facts tofauti zinazowalazimu wabadilishe misimamo yao ili waweze kuendeleza
kuwa Viongozi. Mibiginyo hii inamkumba kila kiongozi bila kujali ukubwa na
nguvu ya nchi anayoiongoza!!
Kila mmoja anaweza kuihisi hali hii katika nafasi yoyote ya
uongozi wa kijamii aliyowahi kuisimamia.
Kundi la pili : MATAJIRI WAKUBWA.
Sifa kuu za kundi hili ni : KUPATA WAKITAKACHO BILA KUJALI NJIA ILIYOTUMIKA
Hawa ni watekelezaji wakuu wa Machiavellism “End justifies the means” . Ukiangalia
kwa makini vita na maafa mengi duniani yamechochewa na kundi hili ambalo lina
nguvu kubwa ya kichinichini katika
kulilazimisha kundi la kwanza (wanasiasa )ili lichukue maamuzi yatayolingana na
matakwa na maslahi yao.
Hili ni kundi pekee ambalo wahusika wake HAWAJIFICHI katika kuhakikisha wanapata wakitakacho.Misimamo
yao ipo wazi mno na wala haina mizunguko.Hawatumii unafiki wa maadili kama wanavyofanya wahusika wa kundi la kwanza
(wanasiasa)na wa kundi la tatu “A” kama tutavyoona hapo mbele.
Kundi la tatu :VIONGOZI WA DINI.
Kundi hili linagawanyika katika sehemu mbili kuu.”A” na “B”.Kundi
la .”A”ni lile la wale wanaotumiwa kwa maslahi ya WANASIASA NA MATAJIRI WAKUBWA.Ama
kundi la “B”.ni lile la wale wachache wanaojaribu kufuata dini bila kujali
maslahi ya kundi la kwanza wala la pili.Mara zote kila mmoja hudai kuwa yumo
katika kundi la “B”.Ila huwa si tabu kuwagundua wapi walipo na hasa kama
watatakiwa watoe maamuzi yatayopingana na maslahi ya WANASIASA au MATAJIRI
WAKUBWA.
Sifa kuu za kundi la tatu “A” ni :KUWALAGHAI WAUMINI.
Wahusika wa kundi hili, ndani ya nyoyo zao wana misimamo ya kundi la kwanza na la pili ila wanapokutana na waumini
wao hujilazimisha waonekane kama wapo pamoja nao kumbe sivyo!!!
Sifa kuu za kundi la tatu “B” ni: KUJITENGA AU KUTENGWA.
Wahusika wa kundi hili wamejigawa katika sehemu mbili.Ya
kwanza ni wale waliokwisha gundua kuwa hawawezi kufikisha mafunzo halisi ya
dini zao bila kuingiliwa na makundi makuu niliyokwisha taja hapo nyuma na matokeo yake huamua
KUJITENGA na kutekeleza dini zao bila marumbano.Ama sehemu ya pili ni ile ya
wale wanaoendelea kuamini kuwa wana nafasi ya kuweza kufikisha mafunzo halisi
kwa waumini wao na huendelea kupambana na makundi makuuu na mara nyingi hufikia
KUTENGWA ili wasiharibu maslahi ya wengine!!!
MWISHO nafungia kwa imani ninayoiamini kwa dhati kuwa
tumekuja duniani miaka kadhaa iliyopita na kila mmoja ataondoka baada ya miaka
kadhaa na kuiwacha dunia ikiendelea kama ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita. Katika
kipindi hiki cha miaka kadhaa tunayoishi HATUNA UWEZO WA KUBADILISHA DUNIA BALI
tuna uwezo wa kujaribu KUREKEBISHA BAADHI YA MACHACHE YANAYOTUZUNGUKA KATIKA
JAMII ZETU.
JE TUANZIE WAPI?
TUANZIE HAPA (…………..KUANZA
KUJITAMBUA NA KUONDOKANA NA FIKRA HASI ZILIZOPANDIKIZWA KATIKA VICHWA VYETU(kwa
maslahi ya wachache) KWAMBA SISI WAAFRIKA MUNGU KATUUMBA TUBAKI KATIKA UNYONGE
NA UDHALILI HADI SIKU YA KIYAMA.)TUSITAKE
MABADILIKO YA GHAFLA(ambayo hutukatiksha tamaa tunaposhindwa kuyafikia) TUANZE
KWA KUREKEBISHA MACHACHE NA KUSIFU KILA JEMA LINALOFANYIKA KATIKA JAMII
ZETU.HATA KAMA LITAFANYWA NA TUSIYEMPENDA.
KAYU LIGOPORA
ATHENS – GREECE
27 AUGUST 2013
0 Comments