Habari ambazo zlizopatikana kutoka kwa baadhi ya Watanzania waishio Saint Petersburg, Urusi, ni kwamba Mtanzania aliyeweka makazi yake mjini hapo kwa muda mrefu Ndg. Shabani Japhari ameaga dunia kwa kujinyonga.
Akituma ujumbe huo kupitia mtandao wake wa Facebook, Ndg. Moses Mango, ambaye pia ni mkazi wa muda mrefu wa Mji huo, alisema ” I hate bringing bad news. Kama wengi mlivyosikia, ndugu yetu Shabani ametutoka leo asubuhi kwa kujinyonga. Kwa sie wote hapa, huu ni mzigo mzito sana aliotuachia. Ningeomba wote tuwe pamoja katika kukamilisha shughuli zote zinazotokana na msiba huu. RIP mrefu“, alimalizia kusema Ndg. Mango.
Shabani alifika Urusi miaka ya 80 kama mwanafunzi, na baada ya kuhitimu masomo yake, alibaki mjini Saint Petersburg na kuendelea kujihusisha na masuala mbalimbali ya biashara. Vijana wengi waliokuwa wakifika Urusi ki masomo walimuheshimu na kumchukulia kama kaka, na wengine kumtaka ushauri katika masuala mbalimbali kutokana na uzoefu wake wa Mji.
Marehemu Shabani, ameacha mke na watoto Kandhaa, na dua zetu tunazielekeza kwa familia hiyo, na familia yake nyingine kubwa, iliyopo Tanzania. Kwa hakika wote tumeshtushwa na msiba huu, ambao bado umetuacha na maswali mengi, bila majibu.
0 Comments