Siku ya Jumamosi tarehe 27.04.2013 Watanzania wanaoishi Ujerumani, chini ya mwamvuli wa umoja wao (UTU) waliuhakikishia ulimwengu kuwa neno "MUUNGANO" lina maana kamili kwa maisha ya Mtanzania na binadamu wengine.
Sherehe hizo zilizowakusanya Watanzania na marafiki wa Tazania kutoka kila kona ya Ujerumani, ziliutingisha mji wa Cologne katika usiku usiokwisha wa kusherehekea miaka 49 ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Ali Siwa Naibu balozi wa Tanzania nchini Ujerumani alikuwa mstari wa mbele akiwaongoza Watanzania katika Muungano Day.
Wasanii mbalimbali walitumbuiza jukwaani na kuipeperusha vilivyo bendera ya Tazania.
Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania ujerumani Mh.Mfundo na kamati yake wameahidi kufanya mambo makubwa na kuitangaza Tanzania kwa hali na mali chini ya Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU)
kwa pich zaidi gonga Hapa
0 Comments