Kama ilivyokuwa imepangwa, jana tarehe 25 Feb. 2012 kwenye ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania Italy, mjini Rome, ulifanyika mkutano wa Jumuiya ya Watanzania Roma. Mkutano huu ambao ulikuwa uambatane na uchaguzi wa viongozi wapya ulifana sana japo wanajumuiya hai hawakuwa zaidi ya nusu ya Wanajumuiya wote. Kutokana na kutokuwepo kwa wanajumuiya zaidi ya nusu, wanajumuiya kwa pamoja waliamua kuupeleka uchaguzi mbele mpaka mwishoni mwa mwezi wa nne, ili kuweza kuandaa mazingira mapya yatakayo fanikisha zoezi ili la uchaguzi. Mgeni wa heshima kwenye mkutano huu alikuwepo Kaimu Balozi wa ubalozi wa Tanzania nchini Italy mh. Salvatory Mbilinyi. Kwenye huu mkutano, wanajumuiya kwa Pamoja walijadili maswala mbalimbali ya kujenga jumuiya kama vile, umuhimu wa kushiriki kwenye vikao mbalimbali vya jumuiya, kujitaidi kutoa michango ya jumuiya na mengineyo mengi. Siku chache zijazo, Kamati ya Utendaji ya jumuiya ya Watanzania Rome, itakaa ili kujadili maandalizi ya sherehe ya muungano wa Tanzania itakayofanyika mwishoni mwa mwezi wa nne. Mara tu kamati ya utendaji itakapo kaa mtajulishwa hatua itakayo fuata.
Hapa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Rome, Mh. Leonce Uwandameno (aliyesimama) akifungua mkutano. Kushoto ni Katibu wa Jumuiya Andrew Chole Mhella na kulia ni Mweka Hazina ndugu Awadhi Suleiman.
Hapa uongozi wa Jumuiya ukimkabidhi Bi.Gunhild Mwakangale kadi tatu za uanajumuiya. Kadi mbili zingine atazifikisha kwa Bi. Alice Maimu na Bi. Hadija Omari Mwakangale. Hawa wote wanaishi Sardegna kusini kwa Italy.
Wajumbe wakilisakata KWAITO.
Kama mnavyoona, wajumbe wakiandaa kitu tumbo yapenda.
Mwenyekiti akipata picha ya pamoja na Wanajumuiya.
Hapa Bi Gunhild akisho some love kwa Mjumbe, Bi. Thanner.
Katibu akiwa pamoja na Yakubu.
Katibu akiwa pamoja na wajume.
0 Comments