Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Taarifa ya Msiba wa Bwana Aziz Sheween




Marehemu Aziz Sheween (kushoto) akiwa kwenye mazungumzo ya kikazi na Mwana wa Mfalme wa Saudi Arabia (HRH Prince Alwaleed Bin Talal bin Abdulaziz Alsaud) wakati wa uhai wake.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule, anasikitika kutangaza kifo cha Bw. Aziz Sheween, Afisa Mambo ya Nje Mkuu Daraja la I katika Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, kilichotokea huko Riyadh, Saudi Arabia. Taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuja nyumbani kwa mazishi zinaendelea na pindi zitakapokamilika taarifa rasmi itatolewa. Tunawapa pole familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki, watumishi wa Wizara na wote walioguswa na msiba huu mzito. FOREIGN AFFAIR BLOG

Post a Comment

0 Comments