Jumuiya ya watanzania Ugiriki baada ya kuhakikisha imekamilisha hatua zote za kumwalika Malkia wa Mipasho (KHADIJA KOPA) inapenda kuwafahamisha wale woote waliokuwa na hamu ya kuja Athens kuhudhuria show maalum ya Malikia huyo WASISITE KUJA. Tunawaarifu kuwa hatua zote za viza zimekamilika na tiketi yake pia ipo OK. Atawasili Athens Alhamis jioni na Ijumaa 23/12 kuanzia saa nne usiku hadi alfajir atatumbuiza katika ukumbi wa AXUM uliopo mtaa wa DROSOPOULU 183 kwa kiingilio cha yuro 20 tu.
Tuna mipango ya kumpeleka nchi jirani akatumbuize kabla hajarejea nyumbani wiki ijayo.
(KAYU LIGOPORA)
KATIBU WA JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI
0 Comments