MV Spice
Islanders ilibeba abiria 3,000
Elias Msuya na Jackson
Odoyo, Zanzibar
MELI ya MV Spice Islanders iliyopata ajali mwishoni mwa wiki iliyopita na kusababisha vifo vya takriban watu 200 na majeruhi 619 ambao waliokopolewa, ilibeba abiria 3,000 wakati uwezo wake ni kubeba abiria 600 tu.Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa idadi hiyo kubwa ya abiria, haijumuishi mizigo ambayo kiasi chake bado hakijajulikana.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Fakhi Dadi alisema jana
kuwa mkoa huo umepoteza watu 1,600 katika ajali hiyo, huku Wilaya ya Wete pekee
ikiwa imepoteza watu 1,141.Dadi alisema hayo alipokuwa akizungumza mbele ya
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad
0 Comments