sensei pichani baada ya ushindi wa mpambanaji wake
Sensei katika kujinyoosha kabla ya kuanza kufundisha

moja ya matukio huko nyuma sensei akipanda daraja
Jina langu Naitwa Edgar Kaliboti, nilijiunga na sanaa za mapambano mwaka 1979 katika hekalu la kujilinda lililopo zanaki mjini Dar es salaam. Nilijifunza style ya Okinawa goju ryu karate chini ya mwalimu Nantambu Camara Bomani ambapo nilifanya mazoezi mpaka kufikia ngazi ya mkanda kahawia (brown belt)
Mwaka 1993 niliondoka kuelekea Sydney Australia ambako niliendelea na sanaa za mapambano chini ya sensei Watanabe nilifuzu kupanda ngazi ya mkanda mweusi (black belt) mwishoni mwa mwaka 1994
Baada ya kushiriki katika michuano mingi nilipata kutambua tofauti kati ya sanaa mbali mbali kiuwezo nikaamua kupanua upeo kisanaa,kwa miaka mingi iliyofuatia nilijifunza style nyingine pia kama phillipino Kali, Arnis de mano, boxing, na kick boxing, Aikido na wrestling pamoja na Brazilian Jiu Jitsu na kushiriki katika mashindano mengi ambapo nilijinyakulia medali nyingi na matuzo tofauti ya ushindi!
Kutokana na ushiriki na uzoefu wa miaka mingi kwa sasa hivi Nimebahatika kuwa na nafasi kama mwalimu mkufunzi wa sanaa mbalimbali hapa Sydney hivyo basi nimekuwa nafundisha wapiganaji wa Karate, boxing , Kickboxing, Mixed martial arts,na kupata mafanikio mengi ya ushindi katika mashindano mbalimbali tofauti ya kimataifa.
Mipango ya baadaye ni kujaribu kusaidiana kupanuana kimawazo na kushirikana kuelekezana kiujuzi na waalimu mbali mbali wa michezo ya sanaa za mapambano nyumbani Tanzania ili kuwapa nafasi vijana ya kukuza uwezo na vipaji vya kimichezo na kuinua viwango kwa ujumla!
Sensei Kaliboti ni Mtanzania aneishi nchi Australia akifanya kazi ya ualimu wa sanaa za mapambano. Blog yetu ilipata bahati kufanya mahojiano nae, zaidi tulimuomba atupe maelezo machache kuhusu yeye na libeneke zima la sanaa ya mapambano. Sensei Kaliboti ni mmoja wa wataalamu na hazina ya Taifa letu kama tukiweza kuwatumia wataalam kama hawa basi naamini ndoto zetu za kushiriki mashindano makubwa ya kimataifa na kufanya vizuri inawezekana.
Huu ni muhtasari kuhusu Mtaalam huyu.
Jina langu Naitwa Edgar Kaliboti, nilijiunga na sanaa za mapambano mwaka 1979 katika hekalu la kujilinda lililopo zanaki mjini Dar es salaam. Nilijifunza style ya Okinawa goju ryu karate chini ya mwalimu Nantambu Camara Bomani ambapo nilifanya mazoezi mpaka kufikia ngazi ya mkanda kahawia (brown belt)
Mwaka 1993 niliondoka kuelekea Sydney Australia ambako niliendelea na sanaa za mapambano chini ya sensei Watanabe nilifuzu kupanda ngazi ya mkanda mweusi (black belt) mwishoni mwa mwaka 1994
Baada ya kushiriki katika michuano mingi nilipata kutambua tofauti kati ya sanaa mbali mbali kiuwezo nikaamua kupanua upeo kisanaa,kwa miaka mingi iliyofuatia nilijifunza style nyingine pia kama phillipino Kali, Arnis de mano, boxing, na kick boxing, Aikido na wrestling pamoja na Brazilian Jiu Jitsu na kushiriki katika mashindano mengi ambapo nilijinyakulia medali nyingi na matuzo tofauti ya ushindi!
Kutokana na ushiriki na uzoefu wa miaka mingi kwa sasa hivi Nimebahatika kuwa na nafasi kama mwalimu mkufunzi wa sanaa mbalimbali hapa Sydney hivyo basi nimekuwa nafundisha wapiganaji wa Karate, boxing , Kickboxing, Mixed martial arts,na kupata mafanikio mengi ya ushindi katika mashindano mbalimbali tofauti ya kimataifa.
Mipango ya baadaye ni kujaribu kusaidiana kupanuana kimawazo na kushirikana kuelekezana kiujuzi na waalimu mbali mbali wa michezo ya sanaa za mapambano nyumbani Tanzania ili kuwapa nafasi vijana ya kukuza uwezo na vipaji vya kimichezo na kuinua viwango kwa ujumla!
Mtembelee Sensei katika facebook http://www.facebook.com/#!/media/set/?set=a.1795079558289.2092461.1278696425
4 Comments
Sensei Rumadha
Kalibot anatisha nimewashana nae moto sana dojo zanaki enzi hizo
muulizeni sensei Pambwe anamkumbukaje katika moto wa kumite
Eddy wacha sio mchezo
Big up Kal we 26 man
Yuko mwingine sensei Rumadha Romi yuko USA hebu mtauteni ntakupa contact zake nae moto
Huyu sensei Rumadha alikuwa ni mtu mmoja mpole sana lakini mwenye akili sana katika mbinu za mapambano, alikuwa sio mchoyo wa ujuzi na alinisaidia sana kunifundisha mbinu nyingi za karate kiila mara tulipokutana kufanya mazoezi yetu nje ya Dojo mara nyingi juu ya majumba fulani fulani ya ghorofa hapo Kariakoo!
Pia Na masempai wengi na wanadojo wengi ambao sijawataja majina lakini tulifanya mazoezi makali makali pamoja hapo katika hekalu la kujilinda enzi hizo wote kwa ushirikiano wao pale Dojo walikuwa ni nguzo muhimu iliyonisandia sana kujenga usugu na umahii wa kimichezo !