Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MZOZO WA TANZANIA NA MALAWI

MZOZO WA TANZANIA NA MALAWI

Mara nyingi nchi huingia vitani kwa sababu za tofauti za mipaka kama hizi na hasa wanapochochewa na makampuni makubwa yenye maslahi yao.

Viongozi wetu wa nchi zote mbili inawabidi wawe macho sana ili tusifikie kuingia vitani maana katika nchi zetu za kiafrika ni rahisi sana viongozi kuchochewa (kutoka kwa makampuni yenye maslahi ya kuuendeleza mzozo) na viongozi hao bila kujielewa wakajikuta wanajadili kuilinda na kuitetea nchi KUMBE WANATETETA MASLAHI YA MAKABAILA ILI KULETA VITA.

Nawaomba viongozi wa Tanzania na Malawi wawe macho sana katika kulitatua suala hili.Wajitahidi kutumia diplomasia hadi mwisho na nina hakika watashinda.Na kama wakiona hawawezi basi wajitahidi kulipeleka kwenye mahakama za kimataifa zinazoshughulika na kesi kama hizi.Vita si utatuzi katika mgogoro huu (Please we have many serious problems..We do not have water,we don’t have electricity,etc WE DON’T NEED WAR please.please).

Sisi wananchi wa kawaida hatuna kauli wala uwezo wowote wa kulitatua tatizo hili.Hii ni kazi ya viongozi wakuu wa serikali mbili husika.Sisi kazi yetu ni kuelezea tu rai zetu ambazo mara nyingi hazisikilizwi kutokana na kuwa zinagongana na maslahi ya wale “WENYE UWEZO WA KUAMUA”

Katika mzozo huu hadi sasa nimefurahishwa na msimamo wa Tanzania(siyo kwa sababu mimi ni mtanzania) bali ni kutokana na mfumo wa kiutulivu na busara wanaoutumia katika kulitatua tatizo hili

MUNGU TULINDE WAAFRIKA.MABALAA TULIYONAYO YANATUTOSHA HATUHITAJI MENGINE.

KAYU LIGOPORA

Post a Comment

0 Comments