Blogger Widgets

Newdeal Africa

Thursday, July 5, 2012

WATANZANIA 6 TU WANAMILIKI PESA KULIKO BAJETI YA NCHI NZIMA!!!!!

WATANZANIA 6 TU WANAMILIKI PESA KULIKO BAJETI YA NCHI NZIMA!!!!!

Kuna siku na sisi watanzania tutafikia ile hali ya watu wachache kuelewa kuwa kila wanapoiba na kuficha pesa nje, madhara siyo tu yatawarudia wengine bali hata na wao au familia zao zitaathirika. Kwa mfano nchi inapokuwa haina uwezo wa kutengeneza barabara kutokana na kutokuwa na pesa,basi hata wale wezi waliolimbikiza mapesa nje hawatafaidi kuyaendesha magari yao ya kifahari katika barabara mbovu zenye mashimo.
Kuiba ni jambo linaloeleweka sehemu zote duniani,hata huku katika nchi zilizoendelea kuna wezi na wabadhirifu LAKINI kuna tofauti kubwa kati ya tunavyoiba sisi 99% na tukatumia 1% kujenga nchi na wanavyoiba wenzetu 1% na wakatumia 99% kujenga nchi zao, na ndiyo maana kila siku sisi tunakatishana tamaa na tunarudi nyuma.
Kwa kuwa wizi na ubadhirifu upo katika DNA za viongozi wengi wa Afrika (sisemi wote nasema wengi) , na hawazuiliki ,ni vyema tungewaomba wanapoiba waibe 1% na watuachie 99%.
PLEASE TUWACHIENI 99% ZITASAIDIA PIA FAMILIA ZENU.

KAYU LIGOPORA
ATHENS

soma habari hiichini:


http://www.wavuti.com/4/post/2012/07/viongozi-wafanyabiashara-watoroshea-nje-fedha-zinazozidi-bajeti-ya-serikali-ya-201213

0 comments: