Blogger Widgets

Newdeal Africa

Saturday, February 11, 2012

TANGAZO:MKUTANO WA UCHAGUZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA ROME


Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Rome, unayofuraha kuwajulisheni kuwa siku ya jumamosi tarehe 25 februari 2012 kuanzia saa nane mchana, kutakuwa na mkutano wa uchaguzi wa viongozi wapya wa Jumuiya ya Watanzania Rome. Mkutano huu utafanyika kwenye ukumbi wa ubalozi wa Tanzania Italy, mjini Rome uliopo kwenye mtaa wa Via Cortina d'ampezzo 185. Wanajumuiya hai wote mnaombwa muwasiliane na katibu ndugu Andrew Chole Mhella ili muweze kupata taratibu nzima za Mkutano huu. Mnaweza kumpata katibu kwa e-mail hii watanzaniaroma@yahoo.it. au kwa simu namba 3479094800. Kwa wale ambao wanapenda kuwasilisha majina yao kwaajiri ya kugombea nafasi hizi mnaombwa mtume majina yenu yakiambatanishwa na nafasi ambayo mnataka kugombea kupitia e-mail ya jumuiya hapo juu. Nafasi ni hizi MWENYEKITI, MWENYEKITI MSAIDIZI, KATIBU, KATIBU MSAIDIZI, MWEHA HAZINA NA NAFASI MBILI ZA WAJUMBE.

Kwa maelezo zaidi mnakaribishwa kutembelea official Blog ya Jumuiya hapa www.watanzania-roma.blogspot.com.

0 comments: