Mara kadhaa imeshatokea baadhi ya watanzania kukosa haki zao kwa sababu ya utumiaji wa uraia wa nchi nyingine.Nasi bado kidogo itukumbe hali hiyo tulipomsafirisha marehemu SAIDI HASSAN MGOI (Maarufu kwa jina la Chance.)
Soma barua tuliyoituma Uhamiaji utapata picha kamili ya hali ilivyokuwa.
Nadhani itapendeza kama tutabadilishana mawazo kuhusiana na hii hali ya mihangaiko ya kimaisha ambayo wakati mwingine hulazimu mtanzania ajiandikishe uraia wa nchi nyingine ili aweze ku-survive katika nchi aliyopo,hali ambayo mara nyingi huwa vigumu kwa wale wasioishi katika mazingira yetu kuielewa.
(
KAYU LIGOPORA)
1 Comments