Blogger Widgets

Newdeal Africa

Tuesday, March 19, 2013

SERIKALI YASHAURIWA KUTOA KIPAUMBELE KWA WATANZANIA WAISHIO NJE YA TANZANIA KATIKA UWEKEZAJI

 
Na Waandishi wetu-MAELEZO_Dar es Salaam.
Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano kimataifa imeshauri Serikali kutoa fursa kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi kuja kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali ili kukuza uchumi wetu.

Kauli hiyo imetolewa leo na wajumbe wa Kamati hiyo ilipokutana na
viongozi waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Kimataifa
ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya bajeti ya mwaka 2013/2014

Walisema wakati umefikwa kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi kutowekewa vikwazo katika kupata taarifa muhimu zinazohusu sekta mbalimbali za uchumi ili waweze kuja kuwekeza badala ya fedha zao kukaa nazo nje ya Tanzania.

Waliongeza kuwa ni vema Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ikaunda
Kitengo maalum cha diplomasia ya uchumi kitakachoshirikisha wataalamu
wa sekta mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika utangazaji wa fursa za
uwekezaji nchini kwa ili kuboresha nyanja za uchumi kupitia Watanzania
waishio nje.

Akijibu baadhi ya hoja za wajumbe wa Kamati hiyo Naibu Waziri wa Wizara wa
Mambo ya Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Maalim alisema kuwa
Serikali hivi sasa inaendelea kutangaza fursa mbalimbali ambazo zipo
Tanzania ambapo tayari wawekezaji kutoka Oman wameshaonyesha nia ya
kuwekeza nchini.

Alisemakuwa wawekezaji hao wanakusudia kununua nyama ambapo pia watajenga
machinjio ya kisasa ambayo yatatumika kuchinjia mifugo kabla ya nyama
haijasafirishwa kwenda nje ya Tanzania.

0 comments: