Blogger Widgets

Newdeal Africa

Saturday, March 30, 2013

Mtanzania afia Uwanja wa Ndege nchini China

KIFO CHA KITATANISHI CHA MBONGO CHINA!! NI KIZAAA ZAAAAA!!“Tangu alipofariki madaktari walisema ripoti ingetolewa baada ya siku saba ambazo ziliisha Jumatatu, mpaka sasa hiyo ripoti hatujaipata lakini Mwambata wa Elimu katika Ubalozi wa Tanzania
nadhani atakuwa ameipata kwa sababu ndiye alikuwa akiiwakilisha Tanzania
katika uchunguzi huo,”

 Mwanafunzi wa Kitanzania aliyekuwa akisoma katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Huazhong nchini China, Leonard Peter Tambalu amefariki dunia ghafla katika
mazingira ya kutatanisha wakati akiwa anajiandaa kurejea nchini.

Tambalu aliyekuwa mwaka wa pili katika chuo hicho kilichopo kwenye mji wa
Wuhan, alifikwa na mauti hayo Machi 17 mwaka huu wakati akiwa katika
Uwanja wa Ndege mjini Beijing. Marehemu alikuwa Ofisa Kilimo Mwandamizi
kutoka wilayani Iramba mkoani Singida.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Christina Midelo hakukubali wala kukanusha kuwapo kwa tukio hilo. “Sina taarifa za kifo cha kijana huyo, wanaoweza kuzungumza ni Ubalozi
wa China kwa kuwa ndio waliokuwa wakimsomesha.”
Balozi wa Tanzania nchini China, Philip Marmo, ambaye yupo nchini kutokana na ushiriki
wake katika mapokezi ya Rais wa China, Xi Jinping, alikiri kufahamu
suala hilo. Katibu wa Umoja wa Wanafunzi wanaosoma vyuo mbalimbali
katika mji wa Wuhan (Wtasa), Humphrey Sikauki, alithibitisha kifo cha Tambalu na kwamba mwili wake ulikuwa unafanyiwa uchunguzi na maofisa wa serikali ya China wakishirikiana na wale wa Tanzania.
Tangu alipofariki madaktari walisema ripoti ingetolewa baada ya siku saba
ambazo ziliisha Jumatatu, mpaka sasa hiyo ripoti hatujaipata lakini
Mwambata wa Elimu katika Ubalozi wa Tanzania nadhani atakuwa ameipata
kwa sababu ndiye alikuwa akiiwakilisha Tanzania katika uchunguzi huo,”
alisema Sikauki.
Gazeti hili lilijaribu mara kadhaa kuwasiliana na
Mwambata wa Elimu katika Ubalozi wa Tanzania nchini China, George
Manongi lakini mawasiliano yalikuwa magumu, kutokana kushindwa
kusikilizana.

0 comments: