Blogger Widgets

Newdeal Africa

Saturday, September 22, 2012

FFU wa Ngoma Africa band watimulisha Vumbi ! AFRIKA-MESSE, Bremen

Kikosi kazi cha Ngoma Africa band iliyozoeleka kwa katibia zake za kupagawisha washabiki wa muziki ughaibuni, Jumamosi ya 15.9.2012 kilifanya kweli katika maonyesho makubwa ya biashara ya Afrika-Messe, mjini Bremen,kule Ujerumani,bendi hiyo maarufu ilipanda jukwaani na kufanikiwa kuziteka nyoyo za washabiki kwa mara nyingine tena kwa kuwadatisha akili na muziki wenye raha kamili. CD za bendi hiyo zimekamata nafasi ya juu katika vituo mbali mbali vya Redio ndani na nje ya Ughaibuni,baadhi ya vituo vya radio zikiwamo Redio maarufu nchi Ujeruamani Radio Funkhaus Europa na Radio Mult-Kult ndizo zinarusha kwa fujo nyimbo za Ngoma Africa band, inayoongozwa na kamanda Ras Makunja wa FFU. Unaweza kuwasikiliza pia katika kambi yao at http://www.ngoma-africa.com au www.ngoma-africa.com

0 comments: