Blogger Widgets

Newdeal Africa

Wednesday, June 20, 2012

BALOZI WA TANZANIA NCHINI ITALIA AKABIDHI HATI KWA RAISI WA ITALIA

Balozi wa Tanzania nchini Italy, Eng. Dr. James Alex Msekela, alikabidhi Hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Italy, Mhe. Giorgio Napoletano, hapo tarehe 19 Juni 2012 saa 11.10 jioni katika kasri ya Rais (Quirinale) iliyopo mjini Rome. Katika hafla hiyo fupi, iliyoanza saa 11 kamili za jioni kwa kwa mapokezi rasmi yaliyohusisha pia gwaride la heshima, Balozi Msekela pia alikuwa na mazungumzo mafupi na mweneyeji wake baaada ya hati zake kupokelewa, ambapo pia alifikisha salaam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Balozi wa Tanzania nchini Italy pia ndiye mwakilishi wetu katika nchi za Ugiriki, Uturuki, Slovenia, Croatia, Serbia, Malta, Bosnia na Herzegovina, na Albania. Katika uwanda wa mashirikiano mapana ya kimataifa, Balozi huyu pia anaiwakilisha Tanzania katika FAO, WFP na IFAD, ambayo yote ni mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) yenye makao yake makuu mjini Rome. Balozi wa Tanzania nchini Italy, Eng. Dr. James Alex Msekela, akikabidhi Hati za utambulisho kwa Mh. Giorgio Napoletano, Rais wa Jamhuri ya Italy, jana tarehe 19 Juni 2012 saa 11.10 jioni katika kasri ya Rais ijulikanayo kama ‘Quirinale’.

 Mh. Giorgio Napoletano, Rais wa Jamhuri ya Italy, akimkaribisha Balozi wa Tanzania nchini Italy, Eng. Dr. James Alex Msekela, katika kasri yake iliyopo kati kati ya mji wa Rome. Kasri hiyo inajulikana kama ‘Quirinale’.

 
 Pamoja na Mh. Napoletano, walikuwepo pia; Mkuu wa Itifaki katika kasri hiyo, na washauri wengine wa Rais wa Italy.
  

 Rais wa Jamhuri ya Italy, Mh. Giorgio Napoletano, akipitia Hati za utambulisho wa Balozi wa Tanzania nchini Italy, Eng. Dr. James Alex Msekela. Baadaye Mh. Rais alimkaribisha Balozi ofisini kwake kwa mazungumzo mafupi.

JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA INAUNGANA NA SERIKALI YA ITALIA KWENYE KUMKARIBISHA NA KUMPONGEZA ENG. DR. JAMES MSEKELA NCHINI ITALIA. JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA PIA INAAIDI KUSHIRIKIANA NA MH. BALOZI KWENYE MASWALA MBALI MBALI YA KUJENGA TAIFA LETU LA TANZANIA. 

Picha zote na Quirinale, Rome.

0 comments: