Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MUUNGANO NA JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI

Napokea salam zenu za BIRTHDAY kwa niaba ya watanzania wa Ugiriki tulioweza kuungana na kuendelea kuwa pamoja katika mazingira magumu yanayoendelea kutuzunguka.

Tarehe yetu hii ya kuzaliwa 26/04/1964 ni ya kubuni ,tunaitumia kuonesha umuhimu wa ushirikiano na muungano. Ilitakiwa birthday yetu iwe ile siku tuliyoisajili rasmi Jumuiya yetu katika Mahakama ya Mwanzo ya Athens(J’tatu 16/09/2002)

Kwa sisi watanzania tunaoishi Ugiriki,neno “MUUNGANO” hatulitumii katika ile maana ya kisiasa inayotambulika na wengi,na ndiyo maana katika maisha yetu ya kila siku hatuna UDINI, UKABILA WALA(…….)

Hali hii ya MUUNGANO tumeikuta tangu miaka mingi ya nyuma toka kwa wenzetu waliotutangulia. Miaka ya nyuma wengi walioishi nchi hii walikuwa si wakaazi walioamua kujenga familia kama ilivyo sasa.Kumbukumbu zetu zinaonesha mtoto wa kwanza kuzaliwa nchi hii akiwa na baba na mama wote raia wa Tanzania alizaliwa 12/01/1994!!!!( Siku hiyo ni siku ya MAPINDUZI)

Kwa sisi watanzania wa Ugiriki maneno “Muungano” na “Mapinduzi” yanajikuta moja kwa moja yana maana inayotusukuma katika “KUSHIRIKIANA.” Na huu ushirikiano hauna maana kwamba sisi hatuna kasoro la hasha.Hakuna jamii yoyote duniani iliyokamilika.

Tunapenda kuwashukuru wale wote wanaoendelea kuuendeleza “MUUNGANO” wetu.Na tunawashukuru kwa dhati marafiki zetu wote waliojiunga nasi @ fb.

Tunamuomba Mola atupe afya na uzima na atuepushe na mabalaa. (Amen)

KAYU LIGOPORA

KATIBU WA JUMUIYA

Post a Comment

0 Comments