Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

UFAFANUZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI

UFAFANUZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI KUHUSIANA NA “KILIO CHA WATANZANIA UGIRIKI”

Kuna Mdau wa ugiriki aliandika katika blog ya Michuzi 12/03/2012 ‘Kilio cha watanzania ugiriki” na kulikuwa na maoni tofauti yasiyopungua 25.

Kwanza kabla ya yote kichwa chake cha habari kingependeza kiwe “KILIO CHA MTANZANIA” na siyo “KILIO CHA WATANZANIA”

Pili ,kwa kuwa mtandao umeleta usawa wa mtu au watu kueleza chochote wakitakacho,imekuwa ni ada kwa baadhi ya watu kuelezea fikra zao kwa kutumia ANONYMOYS na wengine wakidai wapo nchi fulani kumbe hawapo kabisa katika nchi hiyo.

Mimi niandikae maelezo haya naitwa KAYU LIGOPORA mkaazi wa Athens ni Katibu wa Jumuiya ya watanzania tuliopo hapa. Napatikana kirahisi kwa email tanzathens@yahoo.com.

Nimelazimika kuuandika ufafanuzi huu baada ya kuombwa na watanzania wengi wanaoishi hapa waliosoma “KILIO CHA WATANZANIA UGIRIKI”

Ni kweli kuna hali ngumu ya kiuchumi ugiriki ukilinganisha na ilivyokuwa zamani.Yeyote ataepinga hali hili hatokuwa mkweli wa maelezo(Na huu ni ukweli pekee katika maelezo ya kilio cha Mdau wa Ugiriki).Isipokuwa mdau aliyeelezea kilio chake ametumia maelezo mengi yasiyokuwa na ukweli ili aweze kuwakinaisha wasomaji wakubaliane na hoja zake.

Kwa mfano

1. Anadai kuna majina ya wageni zaidi ya milioni waliojiandikisha kurudi (akiwemo na yeye) .. Hakuna ukweli wa idadi hiyo kulingana na takwimu za idara husika za hapa.

2. Anadai pa kulala wanashindwa kulipa hadi kuna wengine wanajipeleka hospitali ili walazwe wapate pa kulala!!!! Namnukuu “Imebidi baadhi yetu kuna ambao wamejipatisha vitanda hospitalini ili kuweza angalau kupata sehemu ya kuweka ubavu na chakula”…Hapa sina comment nawaachia wasomaji, ila tu nchi hii huwezi KUJIPATISHA KITANDA HOSPITALI KAMA HUUMWI na hasa ukiwa mgeni!!!

Inakuwa vigumu mno kuwakinaisha wasomaji wenye busara zao kwamba watanzania wa ugiriki kilio chao ni hicho kilichoelezwa na Mdau ANONYMOYS wakati kwamba juzi juzi watanzania haohao walikuwa wanajirusha na KHADIJA KOPA NA MATONYA na wanajiandaa kumleta mwimbaji mwingine katika kipindi cha Pasaka!!!!

Mwisho,inabidi wanaokuja Ughaibuni kutafuta maisha waelewe kuwa katika kutafuta kuna tabu tofauti ambazo zitawakumba na wanabidi wazivumilie. Ingekuwa maisha ni rahisi kama wanavyodhani basi kila mmoja angekuja Ughaibuni na kurudi Afrika akiwa milionea.

KAYU LIGOPORA

KATIBU WA JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI

Post a Comment

1 Comments

Anonymous said…
Maisha ya ughaibuni yanahitaji uvumilivu na utulivu.Hakuna urahisi kama vile wanavyodhani wengine.