Blogger Widgets

Newdeal Africa

Wednesday, February 29, 2012

GREECE:MWILI WA MAREHEMU JAMHURI TUMEUSAFIRISHA LEO.

Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na jitihada zetu tumefanikiwa kumsafirisha marehemu HAROUN ABDALLAH OTHMAN (Maarufu kwa jina la JAMHURI) ili akazikwe nyumbani.Mwili wa Marehemu utawasili Dar Alhamisi 01/03 saa nane na nusu usiku kwa ndege ya Turkish airline (TK603)

Pamoja na hali ngumu inayoendelea kutukabili watanzania tunaoishi ugiriki ugumu huo hau...kuweza kutuzuwia kutekeleza ada na mazowea ya kumsafirisha mtanzania yeyote anaefariki hapa.

Jumuiya ya watanzania ugiriki, inawashukuru wale wote walioshiriki kwa hali na mali katika kumsafirisha mwenzetu.

Tunapenda kutoa shukurani maalum kwa Kaimu Balozi wetu Rome Italy kwa kututumia haraka mno "barua ya uthibitisho" iliyoturahisishia kwa kiasi kikubwa harakati zote za kumsafirisha Marehemu.
Tunamuomba Allah amlaze Marehemu mahala pema peponi.(Amin)

INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUUN

Kayu LigoporaKatibu Mkuu
Jumuiya ya watanzania ugiriki

0 comments: