Blogger Widgets

Newdeal Africa

Sunday, January 15, 2012

MIAKA 48 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR.. UGIRIKIJumuiya ya watanzania ugiriki ilisherehekea miaka 48 ya mapinduzi ya Zanzibar kwenye ofisi ya jumuiya J'mosi 14/02.Tulilazimika kuichelewesha kwa siku mbili kutokana na mihangaiko ya kikazi.

Sherehe zilianza kwa wimbo wa Taifa na kufuatiwa na risala fupi ya Mwenyekiti mwanzilishi wa Jumuiya yetu bw.Suleiman Nassib (DIDOS)ambae alisisitizia umuhimu wa umoja na ushirikiano.

Ilifuatiwa na shukurani za bi.Joan mwakilishi wa kikundi cha wanafunzi wa Holland tuliowakaribisha rasmi katika sherehe yetu.

Baadae mke wa Mwenyekiti Bi Asha Chunda alikata keki maalum ya mapinduzi na bw.Jackson na bi Sandra walitumbuiza na kuchangamsha ukumbi kwa nyimbo zao zilizowanyanyua hata wageni wetu.

Sherehe ziliendelea hadi alfajiri

KAYU LIGOPORA

KATIBU WA JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI0 comments: