Blogger Widgets

Newdeal Africa

Saturday, August 27, 2011

FUTARI YA JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI


Kwa picha zaidi GONGA HAPA

Kama ilivyo kawaida ya watanzania wa ugiriki kila mwezi wa Ramadhani kuandaa futari ya pamoja kwenye ofisi ya jumuiya,na mwaka huu tuliiendeleza ada hii.Tulikutana 27/08 Jumamosi na kila mmoja-bila kubagua- alileta futari aliyoiandaa nyumbani kwake.
Tunamuomba ALLAH atujaalie SWAUMUN MAQBUUL
Tunamuomba M/Mungu atupe uhai na mwakani tuifanikishe zaidi.
Tunamuomba Mola atuzidishie upendo na atuepusha na kila balaa. AMEN
Kwa picha za ziada tembelea fb "serengeti ugiriki"na"watanzania ugiriki"
Kayu Ligopora
Katibu wa jumuiya

Thursday, August 25, 2011

TANGAZOTUNAPENDA KUWATANGAZIA WATANZANIA WOTE WANAOISHI NDANI NA NJE YA TANZANIA KATIKA SIKU ZIJAZO ZA KARIBU TUTAFUNGUA TELEVISHENI. CHANELI YA MUZIKI WA KITANZANIA, KWA JINA LA TANZANIA MUSIC TELEVISION

{TMTV} (WWW.TMTV.CO.TZ)

AMBAYO ITAKUWA INAPATIKA KWENYE MTANDAO,SETILATI,SIMU ZA MKONONI NA VING'AMUZI(DECODER)

CHANELI HII ITAKUWA NA VIPINDI VIFUATAVYO:

1.BONGO BOX
2.SALAMU BOX
3.BENDI ZETU
 4.TAARABU
5.ZILIPENDWA
6.NYIMBO ZA DINI 
7.VIPAJI
8. HABARI ZA MUZIKI
9.SWAHILI HIP-POP
10.NYIMBO ZA UTAMADUNI

ILI KUBORESHA UFANISHI WA CHANELI TUNAOMBA MAPENDEKEZO YENU KUPITIA:

BONYEZA HAPA KWA KUANGALIA CHANELI


KWA KOMPYUTA NYINGINE UTALAZIMIKA KUDOWNLOD  SOFTWARE YA MICROSOFT SILVER LIGHT KWA AJILI YA KUANGALIA TV.

SOFTWARE ITAJITOKEZA KTK SCREEN KWA AJILI YA KUDOWNLOD. 

WENU

UTAWALA
TANZANIA MUSIC TELEVISION

Øverst i skjemaet

Wednesday, August 24, 2011

MAREHEMU ALIYEZUIWA AIRPORT TOKA UGIRIKI
Mara kadhaa imeshatokea baadhi ya watanzania kukosa haki zao kwa sababu ya utumiaji wa uraia wa nchi nyingine.Nasi bado kidogo itukumbe hali hiyo tulipomsafirisha marehemu SAIDI HASSAN MGOI (Maarufu kwa jina la Chance.)
Soma barua tuliyoituma Uhamiaji utapata picha kamili ya hali ilivyokuwa.
Nadhani itapendeza kama tutabadilishana mawazo kuhusiana na hii hali ya mihangaiko ya kimaisha ambayo wakati mwingine hulazimu mtanzania ajiandikishe uraia wa nchi nyingine ili aweze ku-survive katika nchi aliyopo,hali ambayo mara nyingi huwa vigumu kwa wale wasioishi katika mazingira yetu kuielewa.
(KAYU LIGOPORA)

Facebook makes its privacy settings act more like Google+


When Google's not-the-Facebook social network, Google Plus, launched earlier this summer, one thing stood out for many tech pundits: privacy settings. On Facebook, users had to navigate confusing lists on settings pages in order to control seemingly simple and important things, like who could see their photos or status updates or which books they like....read more>>>>>

Thursday, August 18, 2011

SYDNEY AUSTRALIA:MJUE SENSEI KALIBOTI

sensei pichani baada ya ushindi wa mpambanaji wake
Sensei katika kujinyoosha kabla ya kuanza kufundisha
moja ya matukio huko nyuma sensei akipanda daraja
Sensei Edgar Kaliboti
Sensei Kaliboti ni Mtanzania aneishi nchi Australia akifanya kazi ya ualimu wa sanaa za mapambano. Blog yetu ilipata bahati kufanya mahojiano nae, zaidi tulimuomba atupe maelezo machache kuhusu yeye na libeneke zima la sanaa ya mapambano. Sensei Kaliboti ni mmoja wa wataalamu na hazina ya Taifa letu kama tukiweza kuwatumia wataalam kama hawa basi naamini ndoto zetu za kushiriki mashindano makubwa ya kimataifa na kufanya vizuri inawezekana.
Huu ni muhtasari kuhusu Mtaalam huyu.

Jina langu Naitwa Edgar Kaliboti, nilijiunga na sanaa za mapambano mwaka 1979 katika hekalu la kujilinda lililopo zanaki mjini Dar es salaam. Nilijifunza style ya Okinawa goju ryu karate chini ya mwalimu Nantambu Camara Bomani ambapo nilifanya mazoezi mpaka kufikia ngazi ya mkanda kahawia (brown belt)

Mwaka 1993 niliondoka kuelekea Sydney Australia ambako niliendelea na sanaa za mapambano chini ya sensei Watanabe nilifuzu kupanda ngazi ya mkanda mweusi (black belt) mwishoni mwa mwaka 1994

Baada ya kushiriki katika michuano mingi nilipata kutambua tofauti kati ya sanaa mbali mbali kiuwezo nikaamua kupanua upeo kisanaa,kwa miaka mingi iliyofuatia nilijifunza style nyingine pia kama phillipino Kali, Arnis de mano, boxing, na kick boxing, Aikido na wrestling pamoja na Brazilian Jiu Jitsu na kushiriki katika mashindano mengi ambapo nilijinyakulia medali nyingi na matuzo tofauti ya ushindi!

Kutokana na ushiriki na uzoefu wa miaka mingi kwa sasa hivi Nimebahatika kuwa na nafasi kama mwalimu mkufunzi wa sanaa mbalimbali hapa Sydney hivyo basi nimekuwa nafundisha wapiganaji wa Karate, boxing , Kickboxing, Mixed martial arts,na kupata mafanikio mengi ya ushindi katika mashindano mbalimbali tofauti ya kimataifa.
Mipango ya baadaye ni kujaribu kusaidiana kupanuana kimawazo na kushirikana kuelekezana kiujuzi na waalimu mbali mbali wa michezo ya sanaa za mapambano nyumbani Tanzania ili kuwapa nafasi vijana ya kukuza uwezo na vipaji vya kimichezo na kuinua viwango kwa ujumla!

GREECE:SERENGETI


SERENGETI UGIRIKI IKISHIRIKIANA NA MUBABE TUMEFANYA MAANDALIZI YA KUWALETEA MWIMBAJI WA TAARAB MWENYE SIFA YA HALI YA JUU TANZANIA NA AFRIKA MASHARIKI KOTE, MFALME MZEE YUSSUF ATAKUWA HAPA KUTUTUMBUIZA PAMOJA NA KUTUPA BURUDANI YA HALI YA JUU, WOTE MNAKARIBISHWA KIINGILIO EURO 25 TU, MAHALI ITAKUWA AXUM CLUB: I DROSSOPOULOU 183, TAREHE 03/09/2011 FIKA MAPEMA UWAHI UHONDO WOTE...!

WABONGO GREECE


WATANZANIA GREECE WAKIJAZA CONTAINER KUSAIDIA WASIOJEWEZA TANZANIA. Hii ni mifano y a kuigwa kwa Watanzania wote walioko ughaibuni kwani pamoja inawezekana. Blog hii inapenda kuwapongeza Watanzania waishio Ugiriki pamoja na uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Greece kwa jitihada kubwa zinazofanywa. MUNGU IBARIKI TANZANIA!!

Wednesday, August 17, 2011


Zanzibar government to jail 'abusers' of Ramadhan


By Hamoud Sai - The Citizen Correspondent

Zanzibar. The Zanzibar government has asked the police in the Isles to arrest and charge anyone caught eating, drinking, or selling food at daytime during the current month of Ramadhan. 

The order was issued on Tuesday by state minister Mohamed Aboud Mohamed at a press conference held at the Zanzibar Television (TVZ) premises. The order followed complains about an emerging habit where people ate and drank in public. 

He warned: “Anyone eating and drinking in public as well as opening a bar, guest house and restaurant is committing an offence.”Ramadhan is the ninth month of the Islamic calendar, which lasts 29 or 30 days, in which participating Muslims fast or refrain from drinking, eating and sexual intimacy with their partners during daylight.

Asked if the ban on eating, drinking, and operating restaurants and bars wasn’t a violation of human rights, the minister responded that observing the law was part of respecting them.

“Human rights need people to observe land laws and respect culture. We ask non-Muslims and Muslims who are not fasting to respect the majority believers who are doing it in the islands. Christians and Muslims in Zanzibar have been living and respecting each for decades, and the situation should remain so,” Mr Mohammed said.

Most restaurants are closed in Stone Town, but according to the minister some ‘stubborn’ people still run restaurants, and bars during daytime while others drink openly.

Tuesday, August 16, 2011


 

Nice Gonga White Party in Stockholm - Sweden


PRESENTED BY: FREDDYNICE/GONGA
"We actually hanging out together,working together,neighbours,you know kind f down for what ever brothers,then this other day,. we decided doing entertainment business.,as in parties n styles.classy clean,fresshh u know ,.magnificent black flagging,white as we luv parties,.like trully trully luv life.
After the Stockholm White Party 2010, IceBlackMagic 2011 N SPRING BREAK 2011 feat LADY JAY DEE Pulled Off,,,This time niceGONGA again in collabolations with GREY GOOSE VODKA brings to you STHLM ALL WHITE PARTY 2011....HOTTEST PARTY OF THE SUMMER RETURNS FOR SEASON TWO.
All white attire required/Mandotory attire required.
Ladies: Classy & Sophisticated
Gentlemen: Swagger & Smooth
Side note: feel free to accessorize green, yellow, blue, silver..
RSPV: FREDDYNICE+4673 672 4708
FRANK GONGA +255655400411
www.stockholm   whiteparty.blogspot.com

Sunday, August 14, 2011

TEMBELEA NIFAHAMISHE DOT COM

Welcome to NIFAHAMISHE.COM (inform me.com). This is one of many internet-based news publications for Tanzanians and friends living abroad.
The Publication was established in the United Kingdom, in late 2008, NIFAHAMISHE.COM is currently one of Tanzanian’s and friends abroad major news publishers and we are reputed internationally for our quality content.
NIFAHAMISHE.COM aims to disseminate information to Tanzanians and friends in and out of Africa on issues ranging from community development, culture, personal development, inspiration, health and arts, business practices, innovations and opportunities, finance, world affairs etc. Our goal is to make sure that we inform you well so that you are up to date with what is happening not only Africa but also around the world.
Each page is published by the teams of online journalists based in Tanzania and United Kingdom, Much of the material is written by these journalists. Prior to the execution of a security trade based upon the Financial Data, you are advised to consult with your broker or other financial representative to verify pricing information.
Email; info@nifahamishe.com.   GONGA HAPA

Saturday, August 13, 2011

HIV expert jailed for keeping woman as slave in London flat


Rebecca Balira was convicted at Southwark crown court of keeping Tanzanian woman Methodia Mathias as a slave.

An HIV expert has been jailed for keeping a 21-year-old woman as a slave.
Scientist Rebecca Balira, 45, was convicted at Southwark crown court, south London, for keeping Methodia Mathias in servitude. She was sentenced to six months' imprisonment and ordered to pay Mathias £3,000 in compensation.
Mathias, 21, claimed Balira brought her from her native Tanzania. The court heard that Mathias had stayed with Balira's relatives in Dar es Salaam and they paid for her UK visa applications, the third of which was successful, as well as a return flight to Britain. But she claimed that she was kept as a slave in a flat in Thamesmead, south-east London after coming to the UK.
She said on Balira got so angry one occasion that she cut her bra with a pair of scissors and injured her in the process.
Balira maintained that she only pulled on Mathias's bra, causing it to snap, during a row over money missing from a coin box in September last year.
The court heard that Mathias's friend, Beatrice Kosgei, sought help from the charity Kalayaan, which represents migrant domestic workers.
Kate Roberts, from Kalayaan, said: "We are obviously pleased in cases where there is justice for domestic workers ... But cases such as these do highlight our concerns that instances of such abuse will increase if the protections that are currently maintained within the migration domestic worker visa are removed."
Prosecutor Caroline Haughey said Balira had imposed "conditions that ... amounted to slavery and servitude". Balira was cleared of trafficking a person into the UK for exploitation and of common assault.  THE GUARDIANSIKILIZA BONGO RADIO......New Website!!!

BONGO RADIO is a web-based Radio Station Broadcasting LIVE from Chicago, IL -USA. This is the Best Internet Radio Station for Bongo Flava, Hip Hop, Ragga, Muziki Wa Dansi, R&B, Zilipendwa, Sebene, Mduara, Old School Hip Hop and African Music.

BONGO RADIO is one of the most listened to internet radio stations with listeners from all over the world. We are representing Tanzania and the whole of East Africa to the fullest.

Usikose Kusikiliza Bongo Radio Kwa Muziki Mdundo na Wenye Ladha Ya Hali Ya Juu.
GONGA HAPA- BONGO RADIO

Friday, August 12, 2011

JE WAJUA HII?

Hili ni fundisho kwa dada zetu kule nyumbani kwani hao watu wa magharibi na huko Bongo wapo, sasa wasije wakaendeleza libeneke lao kwetu. tuwe makini na serikali yetu iliangalie hili kwani hata hao wanaokwenda Arabuni nako kazi ni hiyo.

Muda wa kufunga na kufungua kwa waishio nchi za kaskazini ya dunia - utata!Kwa sisi tunaofunga na tunaishi nchi za Kaskazini (Norway, Sweden, Denmark, Finland, Iceland, visiwa vya Faeroe, Greenland) tuko kwenye majira ya Kiangazi na huku majira haya mchana ni mrefu na usiku ni mfupi!

Kuraani Tukufu inasema : Baada ya kuyakinisha jua limetua, waliofunga ni lazima juu yao kufuturu (tafsiri ya Sheikh Said Mussa kwenye kitabu chake cha Kiswahili: Saumu na shuruti zake, uk.16). Hii ina maana tunatakiwa kufunga mpaka tutapoona jua limezama! Kipindi hiki huku, kwa hapa Oslo nilipo jua linazama kwenye saa 3 na nusu hadi nne za usiku saa za ulaya ya kati (Saa 4 na nusu hadi tano za usiku za Afrika Mashariki).

Kwa wale wanaoishi kaskazini ya Norway, ndio usiseme. Jua linazama kwenye saa 5 hadi 6 za usiku za ulaya ya kati (CET = Central European Time) au saa 6 hadi 7 za usiku za Afrika Mashariki (EAT = East African Time).  Mwisho wa kula daku huku, ni kwenye saa 9 na dakika 25 za alfajiri au saa 10 na dakika 25 za alfajiri za Afrika Mashariki. Huku Kaskazi ya dunia tumeanza kufunga kwa masaa 18 badala ya masaa 13 ya Makka (kuchwa na kucha kwa jua): Ni masaa mengi.

Kadri siku zinavyoenda, jua taratibu linawahi kuzama na linachelewa kutoka. Lakini mpaka mwezi wa Ramadhani ukiisha, bado mchana utakuwa mrefu ukilinganisha na usiku.  

Waislamu tunaofunga huku tumekuwa tunajiuliza maswali kadhaa wa kadhaa juu ya nyakati za majira ya Kiangazi yalivyo huku kwenye mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, ukilinganisha na nchi Afrika, Asia, Mashariki ya Kati, Marekani ya Kusini na  Kaskazini. Wanatheolojia na wanazuoni wa Kiislam huku wameshindwa kutoa majibu ya ufasaha juu ya majira ya Kiangazi huku (mchana mrefu usiku mfupi) na muda wa kufunga na kula daku. Wanahitilafiana sana.

Imam Senaid Kobilica, Sheikh Mkuu wa Baraza la Waislam Norway (IRN = Islam Råd Norge) amesema juzi kuwa; wataitisha kikao cha Mashehe na Maimam baada ya Ramadhani kwisha ili kujadili utata uliojitokeza wa suala hili. Imam Kobilica anakubaliana na Imam Basim Ghozlan wa msikiti wa Rabita hapa Oslo kuwa watu wanaweza kufuata masaaa 13,5 ya kufunga ya Makka. Wakati Imam Syed Nehmat Shah wa msikiti wa Central Jamaat-e Ahl-e Sunnat na Imam Hafiz Mehboob ur Rehman wa Islamic Cultural Centre hapa Oslo wanasema kuwa lazima waumini wa Kiislam wafuate masaa yaliyoandikwa kwenye Kuraani Tukufu; Kucha na kuchwa kwa jua!

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwakani utaangukia Julai. Na huku hizi nchi za Kaskazini Julai ni katikati ya Kiangazi! Jua linapotea kama saa moja sana sana masaa mawili. Je, itakuwaje kwa wale watakaojaliwa kuufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani?

Manaake itabidi wafunge kama masaa 23 hivi. Kwa wale waishio kuvuka nyuzi za Actic wao itabidi wasifunge, kwani jua huwa halizami kabisa!!!  

Watu mpaka tumefikia kusema kuwa: Wakati dini ya Kislamu inaanza watu waliokuwa wanaishi enzi hizo hawakujua kama kuna nchi huku kaskazini zilizo na majira ambayo ni tofauti na yale yaliyoko huko kulikoanzia Uislam na matokeo yake ndo utata huu tulionao kama kwenye mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu. Wangejua kuwa huku wakati wa majira ya theluji kukoje na wakati wa majira kiangazi kukoje, labda utata huu usingekuwepo.

Ijumaa kareem!

Mwamedi Semboja
Oslo,
Norway.


Thursday, August 11, 2011

ATHENS GREECE:MWILI WA MAREHEMU SAIDI HASSAN MGOI aka CHANCE KUSAFIRISHWA KWA MAZISHI

Baadhi ya Watanzania pichani wakisubiri kumsalia marehemu

Kwa uwezo wa Allah na ushirikiano wa hali ya juu uliopo kati yetu (watanzania wa ugiriki) tumeweza kufanikisha mchango wa kumsafirisha mwenzetu SAIDI HASSAN MGOI (Maarufu kwa jina la CHANCE) ili akazikwe nyumbani. Mwili wa Marehemu utawasili Dar J'mosi13/08 saa NANE NA NUSU USIKU kwa ndege ya shirika la Uturuki.

Marehemu alikoshwa,alikafiniwa na kuswaliwa katika msikiti wa ELSALAAM uliopo Neos Kosmos Athens.Idadi kubwa ya watanzania walihudhuria msikitini.
Taarifa tulizo nazo khs maziko yatafanyika J'pili 14/8 saa saba mchana Tandika Mikoroshini kwa SANDARI ila kwa maelezo kirefu fanyeni mawasiliano na FATUMA dada yake (0718567537) au (0783694736)
Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi Amin.

INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUUN

Kayu Ligopora
KATIBU wa JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI

Wednesday, August 10, 2011

JAPAN:MKUSANYIKO WA WATANZANIA KWA TAFRIJA FUPI YA KIPINDI HIKI CHA SUMMER.

KWA WATANZANIA JAPAN:
Nadhani baadhi yenu mnayo taarifa. Kwa wale ambao hawajapata taarifa, ningependa kuwaarifu kuwa Jumamosi hii, tarehe 13/Aug/2011, kutakuwa na mkusanyiko wa watanzania wote huko maeneo ya Sagamino. Mkusanyiko huu utafanyika kando ya mto (ni kama beach), na kutakuwa na vinywaji, chakula na nyama za kuchoma na muziki. Maandalizi yameshafikia hatua kubwa.
Kiingilio ni Yen 3,000. Wale ambao hawajachanga wanaweza kuchanga kupitia akaunti ya jumuiya ambayo ni hii hapa chini. Mwisho wa kuchanga ni Alhamisi ya wiki hii (Tar 11/ Aug/2011).
Benki: Sumitomo Mitsui Banking Corporation
Tawi: Kunitachi: No. 666
Jina la Akaunti: Tanzanite Society; Msimamizi: Njenga Rashid Omar
Account No. 7916169

Shughuli hii itaanza rasmi saa 6 asubuhi na kuendelea hadi saa 12 jioni. Na kwa wale watakaopenda kuendelea baada ya hapo huenda wakaruhusiwa. Mkusanyiko huu siyo rasmi kwa hiyo hatutakuwa na hotuba zozote mbali na miongozo itakayotolewa pale inapohitajika.
Lengo ni kukusanyika watanzania wote na marafiki zetu wa karibu kujumuika pamoja na kufahamiana, kuongea na kubadilishana mawazo. Mkusanyiko huu umeandaliwa na wenzetu wa Sagamino na Jumuiya yetu Tanzanite, imeuunga mkono kwa kuwa ni moja ya sera zetu ni kuwaweka watanzania wote wanaoishi hapa Japan kuwa pamoja na kuwa na umoja ulioimarika.
Mkuusanyiko huu ni wa watanzania wote bila kutenga wanachama na wasio wanachama wa Tanzanite. Kutakuwa na kitabu cha kujiandikisha kwa wale wataoona wako tayari kujiunga na kutakuwa na kitabu cha kukusanya michango yetu ya mwezi. Malipo haya pia unaweza kulipa moja kwa moja kwenye akaunti yetu na kutujulisha kwa barua pepe.
Kama muda unaruhusu tafadhali usisite kujumuika nasi. Tunasikitika hatukuweza kuandaa utaratibu maalum kwa wenzetu ambao wapo kwenye mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, lakini kama watapenda kuja kujumuika kwa ajili ya kukutana na kufahamiana, wanakaribishwa.
STESHENI YA KARIBU NI SOBUDAEMAE (ODAKYU LINE) Ukifika stesheni piga simu zifuatazo na utapewa maelekezo zaidi. Mkusanyiko huu unafanyika kando ya mto, bahati mbaya hatuna address kwa wale ambao wangependa kutumia navigation za magari yao kuwafikisha hapo. Ukifika na gari mpaka stesheni hii pia tutakuelekeza.
1. Gwakisa : 080-3242-7442
2. Njenga : 090-6305-6041
3. Mwombeki : 080-2258-7587
4. Kidume : 080-3150-9173
5. Pembe : 080-3458-8786

NJENGA, Rashid
Mwenyekiti
Tanzanite Society, Japan

Foreign Tanzanians’ to have resident permits

From FINNIGAN WA SIMBEYE in Dodoma, 30th July 2011

TANZANIANS who have assumed foreign nationalities will get permanent resident permits starting next year as government evaluates the possibility of having a dual citizenship law.

This was said by Home Affairs Minister Shamsi Vuai Nahodha in Parliament on Friday evening while winding up debate relating to his ministry's budget estimates.

Mr Nahodha, who drew a lot of attention from the lawmakers because of presenting his ministry's budget from an ipad tablet, said the permits will allow those seeking dual nationality to enjoy all the rights as nationals except seeking public office. READ MORE

Don´t be fooled with this kind of email!

From: Mr. Kofi Owusu
Phone: +233545501030
Email: kofiowusuicbgh@hotmail.com


Greetings.

I am Mr. Kofi Owusu a branch bank manager here in Ghana. I have the sum of Three Million, Seven Hundred and Fifty Thousand US Dollars (US$3,750,000.00) which I would like to transfer into your account and invest in your country if possible. There is no risk involve because I have putting all modalities in place and it is going to be a bank-to-bank transfer.

I choose you because I cannot be directly involved for I am still working with the bank and as a civil servant I am not permitted to operate foreign account, I hope you can understand my situation and assist me to receive and invest this money properly in your country as this is my only hope. You will get 40% of the total fund as commission for your sympathetic co-operation while 60% will be for me.

I need your immediate response for more details.

With regards,
Mr. Kofi Owusu
Tel: 00233-545501030

Monday, August 8, 2011

DICOTA 2011:

The Embassy of the United Republic of Tanzania in the United States of America and The Diaspora Council of Tanzanians in America (DICOTA) are together, organizing events to mark 50 years of Tanzania’s independence. His Excellency Jakaya Mrisho Kikwete, the President of the United Republic of Tanzania has agreed to grace the occasion.

The highlight of the cerebrations will be the 3rd DICOTA’s Convention and Uhuru Gala Dinner. The theme of the convention is “Tanzanians in the Diaspora after 50 years of independence”. Tanzanians in the diaspora are most welcome. Other attendees will include individuals with ties to or interest in Tanzania, international organizations, government and business leaders from Tanzania and United States, NGOs and Civil Society Organizations.Venue:

Marriott Washington Dulles Airport hotel
45020 Aviation Drive
Dulles, Virginia 20166, USA.
1-703-471-9500• Fax: 1-703-661-8714
Ample Parking Space available

Booking Information
Dates:

September 22-25, 2011Agenda:

Coming Soon

Registration:

Click Here to Register

WABONGO OSLO WAKIKARIBISHA SUMMER

barbequing at Sognsvannet Oslo 25th June 2011
By Chama Cha Watanzania Oslo (Gonga hapo kwa picha zaidi)

GREECE:TAFRIJA YA KUIAGA TIMU YA TAIFA YA SPECIAL OLYMPICS

Jumuiya ya Watanzania Ugiriki ilifanya tafrija ya kuiaga timu ya taifa ya  special olympic. kwa picha zaidi tembelea facebook ya WATANZANIA UGIRIKI

GREECE:HARUSI YA ASHRAF & CHIKU .

Kwa picha zaidi za harusi tembelea facebook ya  WATANZANIA UGIRIKI  Blog ya jamii inawatakia kila la kheri maharusi.

Naishitaki Serikali, Media, Synovate n.k. kwa hadaa ya LoliondoHapo nyuma nilitoa ushuuda wangu kuhusiana na kikombe cha babu. Baada ya kupata kikombe changu, nilirudi zangu DAR. Siku 12 zikapita nikawa situmii ARV's matokeo hali yangu ikawa mbaya sana ikabidi nikimbizwe hospitalini. Ilinibidi kuzirudia ARV na sasa hali yangu imeimarika kiasi. Rafiki yangu, mwenye virusi vya ukimwi naye alienda kwa babu, aliporudi alianza  kutangaza kwamba kapona. matokeo yake hali yake ikawa mbaya ghafla na kufariki dunia.

Nadiriki kusema wazi kwamba  sidhani yupo hata mmoja aliyepona kwa babu. Kule loliondo nilikutana na watu wengi zaidi ya 10 ambao walifariki wakiwa kwenye foleni, na wengi wao kutokana na ugumu wa maisha walisogea umbali mfupi na kuzitupa miili ya ndugu zao. Nashangaa hadi leo serikali haijatoa tamko kuhusu watu wanaopoteza maisha yao loliondo, wala haijatoa tamko rasmi kuhusu tiba ya babu. Mbaya zaidi, Synnovate wamedandia hili sakata kwa kudanganya umma kwamba 78% ya waliokunywa dawa wamepona

Kabla sijaenda loliondo, ndugu zangu  pamoja na marafiki walikatiza sana moyo kwenda, ila kutokana na hali yangu ya kuichungulia mauti, sikuwa na jinsi. Nililazimika kwenda kutafuta tiba ya loliondo. Cha kushangaza zaidi, baadhi ya hawa ndugu na marafiki nao ni waathirika wa virusi vya ukimwi ambao wanatafuta tiba.Wiki chache baadaye, magazeti na vyombo vingine vya habari vilipambwa na viongozi wa kitaifa waliokwenda kwa babu wakionyesha umma kwamba dawa ya babu kweli ilikuwa tiba kwa mafano "Augustino Mrema"  alisema kapona kisukari.

Matokeo yake hata wale waliokuwa wakinikejeli waliondoka na kwenda kwa babu. Hadi naandika hii barua, wawili kati yao wamefariki baada ya kurudi wakiamini wamepona. mwingine kapandwa na ukichaa baada ya hali yake kuzorota zaidi, na mda wowote anaweza kututoka.Bila viongozi wa serikali kwenda loliondo ndugu zangu na mafariki wasingekufa haraka hivi.

Nadiriki kusema kwamba, naifungulia serikali yetu mashtaka kutokana na vifo vya ndugu zangu wawili na marafiki watatu kutokana na kuudanganya umma. Nazifungulia vyombo vya habari vilivyoshirika kuiadaa umma, pamoja na kampuni ya Synnovate ambayo imezidi kuikoroga jamii wakidai kwamba 78% ya waliokunya kikombe cha babu wamepona. Kwanza serikali ilitudanganya ikisema kwamba ingepima  dawa hiyo ya babu na kutujulisha kama kweli inatibu magonjwa sugu anayodai babu. 

Hadi leo serikali imekaa kimya. Viongozi wengi wa kitaifa wamekimbilia loliondo, kitu ambacho kiliwafanya ndugu zangu ambao hali yao ilikuwa nzuri kuamini kwamba, kama viongozi wanakimbilia loliondo basi nao waende ili wapone, matokeo yake wakafa. Kwa maana hiyo naifungulia serikali makosa mengi ya jinai na udanganyifu. Navishtaki vyombo vya habari pamoja na serikali  kwa kutokuwajali wananchi wake. Nakumbuka Maggid Mjengwa, John Mashaka, pamoja na kaka mmoja anayeitwa Mwilima walileta mijadala  mikali sana kuhusiana na loliondo tukidhania serikali ingechukua jukumu la kuiambia umma ukweli kuhusiana na loliondo ambalo limegeuka kuwa machinjo ya watanzania wasio na hatia.

mdau

Sunday, August 7, 2011

MSIBA GREECE
Jumuiya ya Watanzania Ugiriki (Greece) inasikitika kutangaza kifo cha mwenzetu

SAIDI HASSAN MGOI  (pichani) (Maarufu kwa jina la CHANCE)kilichotokea hospitali ya mjini Piraeus J'tatu 1/8/2011. Marehemu kabla ya kuwasili ugiriki alikuwa ni mkaazi wa Tandika Dar.Hivi sasa tupo katika harakati za michango ya kutuwezesha kumsafirisha nyumbani.

Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi Amin.

INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUUN

Kayu Ligopora
KATIBU

Saturday, August 6, 2011

Kondoo mwenye Korani azaliwa

KIJIJI cha Uduru wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kimegeuka eneo la utalii baada ya waumini wa madhehebu ya Kiislamu kutoka maeneo mbalimbali wilayani humo na maeneo jirani, kwenda kumshuhudia kondoo aliyezaliwa ameandikwa maneno mwilini kwa lugha ya Kiarabu.

Waumini hao walifurika kijijini hapo juzi baada ya sala ya Ijumaa kumshuhudia kondoo huyo aliyezaliwa wiki tatu zilizopita na kuacha watu midomo wazi kutokana na kuwa na maandishi yanayosomeka kiarabu ubavuni, yakitafsiriwa kwa Kiswahili kama Yasini.

Kondoo huyo aliyezaliwa katika familia moja ya waumini wa dini ya Kikristo, aliwavuta waumini wengi kijijini hapo na kutoka nje ya wilaya na mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la ajabu na la kihistoria ambalo halijawahi kutokea.

Akizungumza na HABARILEO Jumapili kijijini hapo, mmiliki wa kondoo huyo, Grace Massawe (55) alisema kondoo huyo alizaliwa takribani wiki tatu zilizopita na hakuwahi kutambua kwamba beberu huyo alikuwa na maandishi hayo, kutokana na kutotolewa nje na mama yake.

Grace alisema baada ya kondoo huyo kuzaliwa, mama yake alibadilisha tabia na kukaa ndani ambapo awali alikuwa akila chakula nje na wenzake, lakini aligundua maandishi hayo baada ya kumtoa nje mwenyewe.

Alisema awali aliona herufi ya W yenye rangi ya dhahabu, lakini siku zilivyozidi kwenda neno hilo lilizidi kukua na kubadilika rangi na kuwa jeupe zaidi, hali iliyompa wasiwasi na kutafuta msaada ili kutambua maana ya maandishi hayo kutoka kwa waumini wa Kiislamu.

“Baada ya waumini wa Kiislamu kufika hapa nyumbani walibaini maandishi hayo ubavuni mwa kondoo huyo kuwa ya Kiarabu yanayosomeka kuwa Yasini,” alisema Grace.

Alisema waumini hao walimweleza kuwa neno hilo ni muhimu sana katika Kitabu Kitakatifu cha Korani, ambalo ni kama kitovu cha kitabu hicho, pia ni moja ya sura muhimu ndani ya kitabu hicho.

Katika hatua nyingine, Grace alisema katika ufugaji wake wa kondoo hakujawahi kutokea tukio la ajabu kama hilo na kueleza kuwa kondoo aliyemzaa alikuwa ni uzao wake wa mara ya pili ambapo awali alizaa kondoo wa kawaida.

Alisema kutokana na kondoo huyo kuvuta hisia za watu wengi, pia viongozi wakubwa wa dini hiyo walifika kushuhudia maajabu hayo, akiwamo Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu  Tanzania (Bakwata) wa Mkoa wa Kilimanjaro, Shehe Rashid Mallya, na Shehe Mkuu wa Wilaya ya Hai, Juma Lyimo.

Baadhi ya waumini waliofika kumshuhudia kondoo huyo na kuzungumza na gazeti hili Aman Ramadhan na Yacoub Mushi wa Lyamungo, walisema tukio hilo ni muujiza wa Mungu uliojitokeza, hususan kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Juhudi za kumtafuta Shehe Mallya kuzungumzia tukio hilo, zilishindikana baada ya simu yake kuita bila kupokewa.

Chanzo: Gazeti la Habari Leo.


Thursday, August 4, 2011

ITALY:Chama cha Mashabiki wa Bao cha Kimataifa

KWA WADAU WA UGHAIBUNI NA NYUMBANI WENYE UJUZI WA MCHEZO WA BAO

KIBA (Klubo internacia de Bao-amantoj)inaandaa Mashindano ya Kimataifa ya Nne ya Mchezo wa Bao

KIBA (Klubo internacia de Bao-amantoj) inakualika kucheza Bao la Kiswahili katika nchi nje ya Afrika.
Anayetaka kushiriki katika mashindano haya hatakiwa kuwa mwanachama wa chama chochote. Wachezaji watawekwa katika makundi mbalimbali kulingana na fani zao. Ukiwa bado mwanafunzi wa mchezo huu, usikose nafasi hii ya kukutana na wachezaji wengine na ya kujifurahisha wakati wa tamasha la GiocaRoma 2011. Tembelea tovuti ya KIBA ukitaka kucheza kwa njia ya barua pepe na kufanya mazoezi.
Tarehe za mashindano:
Septemba 10-11, 2011.
Mahali pa mashindano:
Chama cha Michezo (Associazione Sportiva) Moon River
Via Angelo Battelli, 6
Roma
Italia
Ada:

Bado hatuna hakakia kama unatakiwa kulipa ada, lakini kama ada ikitakuwepo haitazidi yuro 5. Mapato yatatumika kwa miradi ya Changamano ONLUS ya kusaidia watu duni wa Tanzania.

Tarehe ya mwisho ya kujishirika:
Hamna tarehe ya mwisho ya kujishirika, lakini tunaomba wale wanaotaka kujishirika watuandikie mapema ili tuweze kupanga mashindano vizuri zaidi.

Kujishirika: Inawezekana kujiandikishia mashindano katika tovuti ya GiocaRoma: http://www.giocaroma.it/calendario.php, bonyeza kibonyezo "Prenota".

Muundo wa mashindano:
Muda wa kila mchezo hautaweza kuzidi dakika 90.
Zitakuwepo raundi mbalimbali kulingana na idadi ya wachezaji, lakini hazitakuwa kuliko ya tisa.
Wachezaji watapangwa kulingana na Mfumo wa Kiswisi.
Michezo ya raundi itachezwa kwa wakati mmoja.
Kalenda ya raundi itakuwa kama inavyofuata:
Jumamosi, Septemba 10:
04:00 - 05:30 : raundi ya 1
05:30 - 07:00 : raundi ya 2
Chakula cha mchana 07:00-07:30
08:00 - 09:30 : raundi ya 3
09:30 - 11:00 : raundi ya 4
11:00 - 12:30 : raundi ya 5

Jumapili, Septemba 11:
04:00 - 05:30 : raundi ya 6
05:30 - 07:00 : raundi ya 7
Chakula cha mchana 07:00-07:30
08:00 - 09:30 : raundi ya 8
09:30 - 11:00 : raundi ya 9
12:00 : Utoaj rasmi wa matuzo

Matuzo:

Tuzo la 1 halijachaguliwa
Tuzo la 2 hati
Tuzo la 3 hati

Maelezo zaidi:
Ili kupata maelezo mengine na kujiandikisha tafadhali andika kwa info@tavolando.net au info@kibao.org au info@changamano.org.

Tuesday, August 2, 2011

MTANZANIA AGEUZWA MTUMWA NA MTANZANIA

                                      Scientist ‘kept girl of 21 as a slave’
A SCIENTIFIC researcher used a 21-year-old she flew in from Africa as her unpaid slave, a court heard yesterday.
Rebecca Balira is alleged to have forced Methodia Mathias to cook, clean and wash for her while using her as a nanny to her three kids.
The Tanzanian had been promised a £96-a-month salary, but was never paid, London's Southwark Crown Court heard. Jurors were told she was punched when she displeased her boss.
The court also heard that Ms Mathias was stripped of her passport and banned from contacting family or friends.
Her six-month ordeal only ended when she eventually opened up to a friend and police were called in to investigate.
Caroline Haughey, prosecuting, told the court: "She was required to get up at 5am in the morning and prepare both breakfast and lunch for Mrs Balira, then upon Mrs Balira's departure she was required to wake and tend the children, take
the two eldest to school, look after the youngest, clean the house, take the youngest to nursery in the afternoon, wash the clothes by hand, collect the children, cook the evening meal for the children, and then separately for Balira.
"She would then finish the housework going to bed late into the night often 11.30 or midnight.
"During this time Ms Mathias did not receive a penny for her work nor did she have a day off work save on Sunday mornings when she was permitted to attend church."
The court also heard that Ms Mathias had to walk home after the service while Balira and her kids to the bus.
Balira, 47, of Thamesmead, South London, is studying at the London School of Hygiene and Tropical Medicine. She denies trafficking a person for exploitation and holding another in servitude. Case continues.
THE SUNTuesday, 2 August 2011