Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

WATANZANIA ITALY WAFURAHIA KWA PAMOJA SHEREHE YA MIAKA 50 YA UHURU

Kaimu Balozi Mh. Salvator Mbilinyi akikata keki ya miaka
50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Lady Judy akikatakata keki tayari kusambazwa wa Watanzania.

Lady Esther na Lady Lily wakiifungua keki kwautaratiiiiiiiiiiibu.

Hii ndio keki ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara iliyokuwa designed na
ndugu Andrew Chole Mhella, katibu wa Jumuiya ya Watanzania .

Mzee Jabiri akituandalia nyama choma.
Mzuka uliwapanda pia wenyeji wetu ukumbini.
Kushoto ni kaimu balozi, katikati ni mdau tokea Napoli na kushoto ni Mr.
Fungameza wakisakata rumba.
Katibu wa Watanzania Modena Mh. Mwinyimwaka akipeana mkono
wa ongera na Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome mh. Andrew
Chole Mhella.

Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Rome, Mh. Ayoub akipendelea mezani.
Dj Khalifa all the way from Munich German akiwa na Mjumbe Bakari
na Katibu Andrew Chole Mhella.
Baraka Chiririti mdau mkubwa kutoka Siena alikuwepo pia kusherekea na Watanzania
wenzake mjini Rome.
Katibu wa Jumuiya Mr.A. Mhella kulia akiwa na mdau ndugu
Yakubu Kipwate.
Flowers kutokea napoli wakiongozwa na Lady Judy wakijipatia msosi..

Ile sherehe ambayo ilikuwa inasubiliwa na Watanzania wote nchini Italy, ilifanyika siku ya ijumaa tarehe 9 Disemba 2011. Sherehe ilipambwa na Watanzania kutoka sehemu mbalimbali za Italy kama vile Rome, Modena, Napoli, Siena na sehemu zingine na pia kuudhuliwa na wageni kadhaa kutoka nchi rafiki za Tanzania. Mgeni wa heshima alikuwa Kaimu Balozi, Mh. Salvator Mbilinyi ambaye aliambatana na maafisa wote wa ubalozi wa Tanzania nchini Italy. Sherehe ilianza kwa kuimba wimbo wa Taifa na baadae mgeni wa heshima Kaimu Balozi Mh. Salvator Mbilinyi kufungua rasmi. Kaimu balozi alianza kwanza kwa kuelezea umuhimu wa kusherekea siku hii ya miaka 50 ya uhuru. Baada ya hapo alielezea kidogo juu ya upatikanaji wa uhuru wa Tanzania toka kwa wakoloni wa kiingereza. Mh. Kaimu balozi aliwashukuru pia Watanzania wote kwa ushirikiano wao walioonyeshe kwenye kuiandaa siku hii muhimu zaidi viongozi wa Jumuiya mbalimbali za watanzania hapa Italy kwa kuweza kukusanya michango mbalimbali ambayo imeweza kufanikisha sherehe hizi. Mungu Ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
GONGA HAPA KWA PICHA ZAIDI- PICHA

Post a Comment

0 Comments