Blogger Widgets

Newdeal Africa

Monday, December 26, 2011

KOPA ATEMBELEA OFISI YA JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI


Baada ya kumaliza kutumbuiza Amsterdam na Napoli, bi Kopa alirejea tena Athens 26/12 na kukutana na watanzania pamoja na watoto wao katika ofisi ya jumuiya.

Alipomaliza kusaini kitabu cha wageni bi Kopa alielezea furaha yake jinsi tulivyompokea na alipendezeshwa mno na umoja wetu.”Ukweli furaha yangu haielezeki kwa maneno na nimeridhishwa mno na jinsi mnavyoishi na hasa kuwa na jumuiya iliyopangika kama hii”Aliyasema hayo baada ya kutembezwa katika eneo la Serengeti sehemu yenye michezo ya pool na kantini ya jumuiya.

Na kabla hajaondoka alikabidhiwa zawadi ya jumuiya toka kwa Katibu bw.Kayu Ligopora ambaye alimshukuru bi Kopa kwa jinsi alivyowafurahisha watanzania wa Ugiriki ambao wengi wao walihitaji aje tena mwakani.0 comments: