Blogger Widgets

Newdeal Africa

Thursday, August 11, 2011

ATHENS GREECE:MWILI WA MAREHEMU SAIDI HASSAN MGOI aka CHANCE KUSAFIRISHWA KWA MAZISHI

Baadhi ya Watanzania pichani wakisubiri kumsalia marehemu

Kwa uwezo wa Allah na ushirikiano wa hali ya juu uliopo kati yetu (watanzania wa ugiriki) tumeweza kufanikisha mchango wa kumsafirisha mwenzetu SAIDI HASSAN MGOI (Maarufu kwa jina la CHANCE) ili akazikwe nyumbani. Mwili wa Marehemu utawasili Dar J'mosi13/08 saa NANE NA NUSU USIKU kwa ndege ya shirika la Uturuki.

Marehemu alikoshwa,alikafiniwa na kuswaliwa katika msikiti wa ELSALAAM uliopo Neos Kosmos Athens.Idadi kubwa ya watanzania walihudhuria msikitini.
Taarifa tulizo nazo khs maziko yatafanyika J'pili 14/8 saa saba mchana Tandika Mikoroshini kwa SANDARI ila kwa maelezo kirefu fanyeni mawasiliano na FATUMA dada yake (0718567537) au (0783694736)
Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi Amin.

INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUUN

Kayu Ligopora
KATIBU wa JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI

1 comments:

Anonymous said...

Mungu amlaze mahala pema peponi na azidi kuwapa moyo wa upendo na ushirikano ndugu zetu wa ugiriki