Blogger Widgets

Newdeal Africa

Thursday, August 4, 2011

ITALY:Chama cha Mashabiki wa Bao cha Kimataifa

KWA WADAU WA UGHAIBUNI NA NYUMBANI WENYE UJUZI WA MCHEZO WA BAO

KIBA (Klubo internacia de Bao-amantoj)inaandaa Mashindano ya Kimataifa ya Nne ya Mchezo wa Bao

KIBA (Klubo internacia de Bao-amantoj) inakualika kucheza Bao la Kiswahili katika nchi nje ya Afrika.
Anayetaka kushiriki katika mashindano haya hatakiwa kuwa mwanachama wa chama chochote. Wachezaji watawekwa katika makundi mbalimbali kulingana na fani zao. Ukiwa bado mwanafunzi wa mchezo huu, usikose nafasi hii ya kukutana na wachezaji wengine na ya kujifurahisha wakati wa tamasha la GiocaRoma 2011. Tembelea tovuti ya KIBA ukitaka kucheza kwa njia ya barua pepe na kufanya mazoezi.
Tarehe za mashindano:
Septemba 10-11, 2011.
Mahali pa mashindano:
Chama cha Michezo (Associazione Sportiva) Moon River
Via Angelo Battelli, 6
Roma
Italia
Ada:

Bado hatuna hakakia kama unatakiwa kulipa ada, lakini kama ada ikitakuwepo haitazidi yuro 5. Mapato yatatumika kwa miradi ya Changamano ONLUS ya kusaidia watu duni wa Tanzania.

Tarehe ya mwisho ya kujishirika:
Hamna tarehe ya mwisho ya kujishirika, lakini tunaomba wale wanaotaka kujishirika watuandikie mapema ili tuweze kupanga mashindano vizuri zaidi.

Kujishirika: Inawezekana kujiandikishia mashindano katika tovuti ya GiocaRoma: http://www.giocaroma.it/calendario.php, bonyeza kibonyezo "Prenota".

Muundo wa mashindano:
Muda wa kila mchezo hautaweza kuzidi dakika 90.
Zitakuwepo raundi mbalimbali kulingana na idadi ya wachezaji, lakini hazitakuwa kuliko ya tisa.
Wachezaji watapangwa kulingana na Mfumo wa Kiswisi.
Michezo ya raundi itachezwa kwa wakati mmoja.
Kalenda ya raundi itakuwa kama inavyofuata:
Jumamosi, Septemba 10:
04:00 - 05:30 : raundi ya 1
05:30 - 07:00 : raundi ya 2
Chakula cha mchana 07:00-07:30
08:00 - 09:30 : raundi ya 3
09:30 - 11:00 : raundi ya 4
11:00 - 12:30 : raundi ya 5

Jumapili, Septemba 11:
04:00 - 05:30 : raundi ya 6
05:30 - 07:00 : raundi ya 7
Chakula cha mchana 07:00-07:30
08:00 - 09:30 : raundi ya 8
09:30 - 11:00 : raundi ya 9
12:00 : Utoaj rasmi wa matuzo

Matuzo:

Tuzo la 1 halijachaguliwa
Tuzo la 2 hati
Tuzo la 3 hati

Maelezo zaidi:
Ili kupata maelezo mengine na kujiandikisha tafadhali andika kwa info@tavolando.net au info@kibao.org au info@changamano.org.

0 comments: